Kabla ya elimu ya bure mwakani naomba kujua haya

FATHER OF HISTORY

JF-Expert Member
Joined
Aug 15, 2012
Posts
915
Reaction score
638
Niliposikia rais akitangaza kuwa kuanzia mwakani elimu nchini itakuwa bure nilijiuliza maswali haya:

1. Mbona kuna wanafunzi wengi mpaka sasa matokeo yao ya mitihani yamezuiliwa serikali haija wasaidia?

2. Mbona walijaribu kufuta ada ya mitihani wakashindwa na badala yake adazimekuwa maradufu?

3. Kwanini wasianze kufuta ada ya mitihani ambayo ni kubwa kuliko ada ya shule hususani shule za kata?

Mfano:Ada ya Mtihani kidato cha nne na sita ni 50,000/= Kidato cha Pili; 20,000/= wakati ada ya mwaka ni 20,000 kwa shule za kata baadhi ya wazazi bado hawalipi.

4. Mbona hatuoni ajira za walinzi,wapishi mashuleni hasa zile za kata,je serikali itawalipia mishahara pia?

5. Mbona hatuoni Madawati yakiandaliwa kupelekwa mashuleni kwaajili ya wanafunzi wa mwaka wa kwanza?
Isije ikawa ada inafutwa michango yote ikahamia kwa wazazi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…