Kabla ya kuanza kufanya marketing jiulize maswali yafuatayo

Kabla ya kuanza kufanya marketing jiulize maswali yafuatayo

Elisha Chuma

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2013
Posts
282
Reaction score
275
[FONT=Times, Times New Roman, serif]Marketing kwa maana moja mimi huwa naiita ni zao la Branding kwenye biashara ambalo linatakiwa litoke liende kuitangaza brand iliyojitengeneza.Hapa nchini biashara nyingi zinafanyika kwa mazoea na watu wanafanya bila kuelewa au kuwa na maana halisi ya kitu wanachokifanya, utakuta mtu ameona kampuni fulani wamefanya kitu fulani kwa ajili ya bidhaa, biashara au huduma kwa ajili ya kampuni yao, basi na yeye pia atataka kubadilisha jina tu kwenye hicho kitu kutoka jina la biashara alioiona hadi jina la biashara yake, ila vingine ataviaacha kama vya mwenzake kwa vile tu amependa jinsi kile kitu kilivyo. Na wengine hufanya hivyo kwa mifano na kujaribu .
[/FONT]




[FONT=Times, Times New Roman, serif]Leo nitaelezea kidogo vitu vya kuzingatia kabla hujaanza kujitangaza au kufanya marketing,Tutaangalia vitu kama vitano(5) ambavyo unatakiwa kuviangalia kwenye biashara yako kabla ya kuanza kufanya marketing, vitu hivi mara zote huwa ni vitu vya kawaida na huonekana ni sio vya muhimu sana lakini nikupe siri ndugu yangu hakuna kitu ambacho sio cha muhimu hata kama ni kidogo kiasi gani.
[/FONT]





  1. [FONT=Times, Times New Roman, serif]Uko kwenye biashara gani?[/FONT]
[FONT=Times, Times New Roman, serif]Kabla ya kufanya marketing lazima utambue uko katika biashara ya aina gani, kuna biashara za aina mbili huduma na bidhaa.Njia zake za kufanya marketing (kutafuta masoko) zinatofautiana japo soko ni moja, kila biashara huwa inamtafuta mteja, mfano wa biashara zinazotoa huduma ni kama Washauri, Mahospitalini, n.k na biashara zinatoa bidhaa ni kama Makampuni ya vinywaji, Maduka n.k . Hivyo hata katika mbinu za utafutaji wake wa masoko zinakuwa tofauti, mbali na kutambua aina ya biashara ni lazima hapo hapo utambue na njia zake za kuingiza na kutoa pesa
[/FONT]





  1. [FONT=Times, Times New Roman, serif]Malengo yangu ni yapi?[/FONT]
[FONT=Times, Times New Roman, serif]Baada ya kutambua aina yako ya biashara sasa unakuja hatua ya pili ambayo ni kutambua malengo, katika biashara malengo ni kitu cha muhimu na asilimia kubwa ya biashara zinazofanikiwa ni kwa sababu zimesimamia malengo na kuhakikisha yanafikiwa. Hivyo ni lazima biashara iwe na malengo na sio kampuni peke yake bali kila kinachofanyika ndani na nje ya biashara ni lazima kiwe na lengo ama malengo ambayo hayatakiwi kuwa na mwisho unaotofautiana.
[/FONT]





  1. [FONT=Times, Times New Roman, serif]Nnatoa faida gani?[/FONT]
[FONT=Times, Times New Roman, serif]Faida pia ni kitu kingine kikubwa ambacho kinaongozwa na marketing na mauzo hivyo kabla ya kuingia katika kutafuta masoko inabidi kwanza utambue unatoa faida gani kwa biashara unayoifanya na unataka ikupe matokeo gani? na wewe mwenyewe na biashara mnatoa faida gani kwa mtumiaji wa mwisho na iwapo wewe ndio ungekuwa mtumija wa mwisho ungependa bidhaa au huduma itoleweje?.
[/FONT]

[FONT=Times, Times New Roman, serif]

[/FONT]

[FONT=Times, Times New Roman, serif] 4 . Nini ni faida nilizonazo kwenye ushindani?
[/FONT]

[FONT=Times, Times New Roman, serif]Kabla ya kuingia katika ushindani sokoni ni lazima pia uangalie faida za ushindani, ambapo faida za ushindani ni kwako ni udhaifu wa mshindani ,sio tu kuanzisha kampeni kwa vile mwenzako ametengeneza kitu kama kile na wewe ufanye kwa kutegemea matokeo sawia, angalia kwanza unafaida gani za kiushindani na unazitumia vipi hapo ndio unaweza kufanya kitu ili kikuletee matokeo chanya.
[/FONT]

[FONT=Times, Times New Roman, serif]

[/FONT]

[FONT=Times, Times New Roman, serif] 5. Nnaogopa nini?
[/FONT]

[FONT=Times, Times New Roman, serif]Kama mfanyabiashara au biashara lazima kuna vitu ambavyo utakuwa unaviogopa kwenye soko haijalishi vinaathari kwako au kwenye biashara, vitu hivyo pia vinatakiwa viwekwe hadharani kwa kuzingatia aina ya biashara na kampeni ya masoko unayotaka kuifanya hii itakusaidia kutengeneza njia nzuri za kuviepuka au kutafutia mbinu mbadala ya kuvishinda.
[/FONT]
 
Kaka Elisha big up kwa hii topic. Hapa ndipo biashara zinaweza kuanza, kuendelea na kukua au kinyume chake. Nahisi unavitu vingi kuhusiana na hii kitu ila bado ujafunguka vya kutosha, naomba jiachie kwa manufaa yangu na wengine.
Kingine, mm nadhani branding ni zao LA marketing na sio marketing zao la branding. Naomba tueleweshe.
 
Branding ni picha au muonekano wa biashara yako kwa wateja yaani meseji unayoitaka iwe ndani ya vichwa vya wateja na wateja watarajiwa na marketing ni hali ya kuitoa brand ndani ya ofisi na kuipeleka kwa mteja unaemtarajia, ndio maana kazi ya watu wa marketing ni kutafuta wateja ,unapofanya marketing kwa mtu ni kwamba unafanya kazi ya kuitoa brand ofisini na kuiweka kwenye kichwa cha mteja,muonekano unakuwepo kwanza ndio unaupeleka sokoni, sio unaenda sokoni kutafuta muonekano wako. Na kila kitu kipo ndani ya branding mfano mzuri ni kampuni ya simu ya smart walianza na kampeni za kutafuta kupewa jina kabla ya kuuleta mtandao hewani baada ya kuona jina la smart li afaa kuwatambulisha sokoni ndio wakaliachia na kulifanyia branding nadhani umenipata kidogo hapo mkuu
 
Branding ni picha au muonekano wa biashara yako kwa wateja yaani meseji unayoitaka iwe ndani ya vichwa vya wateja na wateja watarajiwa na marketing ni hali ya kuitoa brand ndani ya ofisi na kuipeleka kwa mteja unaemtarajia, ndio maana kazi ya watu wa marketing ni kutafuta wateja ,unapofanya marketing kwa mtu ni kwamba unafanya kazi ya kuitoa brand ofisini na kuiweka kwenye kichwa cha mteja,muonekano unakuwepo kwanza ndio unaupeleka sokoni, sio unaenda sokoni kutafuta muonekano wako. Na kila kitu kipo ndani ya branding mfano mzuri ni kampuni ya simu ya smart walianza na kampeni za kutafuta kupewa jina kabla ya kuuleta mtandao hewani baada ya kuona jina la smart li afaa kuwatambulisha sokoni ndio wakaliachia na kulifanyia branding nadhani umenipata kidogo hapo mkuu

Yap umeongea safi....
 
Back
Top Bottom