Kabla ya kuchukua uamuzi, fikiri zaidi na zaidi

RIGHT MARKER

Senior Member
Joined
Apr 30, 2018
Posts
129
Reaction score
473
Mhadhara 30:
Aliwahi kusema kiongozi wa zamani wa Ujerumani kwamba:- "Fikiri mara elfu kabla ya kuchukua uamuzi, lakini baada ya kuchukua uamuzi kamwe usirudi nyuma hata ukipata shida elfu"

Je, kuna ukweli wowote juu ya hili?

1. Huenda unataka kung'atuka kwenye ndoa yako kwa sababu ya taabu, shida, mateso, au ushauri kutoka kwa marafiki. Lakini kabla ya kufanya hivyo fikiri mara elfu juu ya uamuzi wako.

2. Huenda unataka kuacha kazi ya kuajiriwa ili ukajiajiri baada ya kuambiwa kuwa kilimo cha Matikiti maji kinalipa, lakini kabla ya kuchukua uamuzi fikiri mara elfu.

Kulingana na maneno ya kiongozi huyo ni kwamba; kabla ya kufanya uamuzi hakikisha unafikiri mara nyingi zaidi ili usije kuingia au kuingizwa choo cha kike. Na kama utaamua kufanya uamuzi usisahau kuwa kila mabadiliko au maamuzi yanakuja na changamoto zake, hivyo kwa sababu ulifikiri mara elfu ndipo ukachukua uamuzi basi hata ukipata changamoto elfu usirudi nyuma.

Right Marker
Dar es salaam
Oktoba 3, 2024
 
Hayana muongozo, kikubwa ni kufuata moyo wako unasema nini basi
 
Back
Top Bottom