Elections 2010 Kabla ya kufikiria ushindi,je unayajua haya?



Hivi una wadhifa gani vile katika kile kitengo cha propaganda cha thithiem? Mpigie kura Rais mtarajiwa Dr Slaa na wagombea ubunge wa chadema. Thithiem na kikwete wameshindwa katika utendaji wa kuiongoza nchi na ushahidi upo wa kutosha tu.
 
Hivi una wadhifa gani vile katika kile kitengo cha propaganda cha thithiem? Mpigie kura Rais mtarajiwa Dr Slaa na wagombea ubunge wa chadema. Thithiem na kikwete wameshindwa katika utendaji wa kuiongoza nchi na ushahidi upo wa kutosha tu.
Mfalme ndugu yangu mimi si mwanachama wa chama chochote, wala sijawahi kuwa mwanachama.
Nakubaliana na wewe CCm hawajafanya vizuri sana katika uongozi, lakini ni ushahidi gani wa kutosha unaoonyesha CHADEMA itashinda?
 
Mfalme ndugu yangu mimi si mwanachama wa chama chochote, wala sijawahi kuwa mwanachama.
Nakubaliana na wewe CCm hawajafanya vizuri sana katika uongozi, lakini ni ushahidi gani wa kutosha unaoonyesha CHADEMA itashinda?

Ushahidi ni kwamba Kikwete na chama chake wameshindwa kutimiza ahadi zao na wapiga kura wengi kusema watabadili upigaji kura wao tofauti na ilivyokuwa 2005. Na pia katika ile mikoa ambayo ina wakazi wengi nchini chadema wanayo mikoa 6, nisingependa kuitaja, wanahitaji mikoa mingine minne tu ili kuhakikisha ushindi wa kishindo na tayari mikoa mitatu inaanza kuegemea zaidi kwa Dr wa kweli. Unafikiri kuzima umeme jana ili Watanzania wasimuone rais wao mtarajiwa ilikuwa bure?
 

Sawa mkuu, kama wamesema,(sijui wapi?) ngoja tusubiri hii wiki moja hiyo mikoa minne ipatikane tuone
 

Si ungefupisha tu na kusema CCM ITASHINDA?Hizi misguided one-sided analyses zinatumika kama propaganda mufilisi za kuwakatisha tamaa wanaotaka mabadiliko.Kwani KANU ilipobwagwa na wapinzani Kenya haikuwa na sifa hizohizo zinazokuaminisha kuwa CCM itashinda kirahisi?
 
Ndugu yangu nakubaliana na wewe kuwa haya maoni yako binafsi hayawezi kutubalisha hata kidogo tumeamua mwaka huu tunafanya mabadiliko makubwa ,na nafurahi kwamba ulifuatilia mdahalo wa jana na umeona jinsi ulivyotikisa nchi nchi nzima ilizizima,mijini na vijijini na hata kwa mara ya kwanza umeingia jamvini kwa njia ya upole ili kuweza kutushawishi tukate tamaa kwamba wakati wa mabadiliko haujafika ,mi nadhani unakosea sana
Katika jamii ya kibinadamu fikra,akili katika mambo ya kijamii huwa yana nyakati ndio maana utaona hata katika nyanja ya kidunia kulikuwa na tawala za mafarao, wafalme wakiyahudi , kirumi,kituruki,kihindi kichina,kiingereza na hizo zote zilianguka,ukweli ni kwamba jamii kwa maana ya watu wanapofikia kuchoka na kitu wanaamua vinginevyo yaani wanaamua kuwa na mabadiliko ili mradi wakiona kuna mtu wanayemwamini mtu ataye weza kuwavusha daraja

Nilikuwepo jana pale movenpick nikiwa katika mdahalo ule nilikuwa nimefunga simu
ulipokwisha niliweza kufungua simu yangu kulikuwa na message 30 na missed calls 18 ambazo kila moja ilikuwa inasema wanamwamnia Dr Slaa na kila mtu akasema atakusanya watu wa rika zote ili ahakikishe wanampa kura ili aweze kutuvusha.katika simu hizo alikuwepo rafiki yangu mmoja ambaye hatujawahi kukutana toka tulivyomaliza darasa la saba na kufaulu kupangiwa shule mabali mabali ambazo zilitutoa kwetu na hata hajuwahi kukutana
katika message akanikumbusha tulivyokuwa darasa la saba tulimwibia mwalimu Ngurumo Pen tukaficha kwenye uzi wa swete niliyovaa mimi,wenzetu kwa kujua utundu wetu walituhisi sisi mwalimu alikagua na kukagua hakuona pen lakini alitucharaza viboko kweli kweli kwa sababu kura ya maoni ya wanafunzi ilituangukia sisi aliniambia tunapaswa kuicharaza viboko CCm kama Mwalimu Ngurumo alivyotucharaza sisi

Rafiki yangu ambaye ni Mkuu wa wilaya moja hapa DSM alinipigia simu akaniambia na washangaa watanzania jinsi munavyomuami Dr Slaa mtu anawaongopea lakini munamwamini kuliko kawaida huyo ni rafiki yangu aliyepewa dhamana na Jakaya kuongoza wilaya yetu anakili kuwa tunaimani sana na Dr Slaa manake ni kuwa kwa imani hiyo watanzania kwa wingi tutampigia kura Dr Slaa,Ukumbuke mimi ni CCM

Nikirudi nyumbani mtaani kwetu nikakuta aliyekuwa mke wa Gavana y Benki kuu miaka iliyopita na kundi la majirani watu wazima kwa vijana kama hamsini walikuwa wanashangilia na kugonga glasi za vinywaji wakisema tumempata mkombozi huyu naye amekulia CCM,mumewe aliwahi kushika wadhifa mkuu hapa nchini kwa miaka mingi
Kufupisha hadithi hii ni kwamba mnyambulisho wa maoni yako unaweza ukawa wa upeo mfupi ukweli watanzania wamebadilika walisha badilika toka mwaka 1995 angeacha mwalimu Nyerer kuuza Mkapa ,mrema angelichukua nchi jiulize kipindi chote hicho

ndugu yangu wakati wa mabadiliko umeshawadia na hii ni kawaida kabisa katika mienendo ya kibinadamu lazima wakati kama huu unatokea hakuna wakuzuia tumwombe Mungu watawala wabadilishane utawala kwa amani ili tuweze kusukuma gurudumu la maendeleo ya nchi yetu mbele
Mungu Ibariki Tanzania
 
Mkuu kama umesoma vizuri post yangu, utajua kuwa sina nia ya kukatisha tamaa wapinzani kama unavyosema wewe,wala post yangu haishawishi mtu yeyote kupigia chama fulani kura,pia sijasema CCm itashinda kirahisi, tathimini yangu inaangalia uwezekano wa makundi ya wapiga kura kwa vyama hivi viwili.
Kuhusu sijui KANU,nahakika unajua ni nini kilifanyika hadi kuiangusha KANU, hivyo nimakosa makubwa kulinganisha siasa za wengine na zetu
.
Ndugu yangu Froida.hivi hii dhana ya kuja kuwakatisha tamaa inatoka wapi?, hayo mabadiliko mliyo amua (sijui na nani?)hata mimi nayataka, swala la muda wa mabadiko liko juu ya wakati na hali halisi ya wakati husika.

Froida kuanguka kwa tawala hakuna fomula, kuanguka kwa british empire si sawa na kuanguka kwa Roman empire,na ndio maana kuanguka kwa KANU si sawa na CCM, hakuna aliyesema CCM itatawala milele, ikfika 2015, tutatoa tathimini kutokana na wakati huo
By the way, hadithi yako inafurahisha masikioni kwa watu wenye matumaini ya CHADEMA kushinda uchaguzi, lakini inawahusu wapiga kura wachahe mno kuliko unavyoweza kufikiri wewe
Nakubali ni mienendo ya binadamu kufanya mabadiliko,lakini unapaswa kuzingatia nyakati na hali halisi ya wakati husika. Ndio maana tunajaribu kutoa hali halisi ili ikiitokea haikuwa ulivyo tegemea wewe basi sababu ulisha pewa.
 

nakugongea Thanx mkuu!
 
Nadhani wewe na mimi tunakubaliana kuwa anayeingia kwenye ushindani lazima awe na matumaini ya Kushinda ni kweli sisi wananchi wengi tuu ( sio wewe ) tunaamini wakati ma mabadiliko umefikia na kuondoa uongozi wa kiimla wa Familia moja na marafiki zao kutuamlia
mambo ya kimstakabali wa nchi yetu kisiasa,kiutawala,kiuchumi na usatawi wa jamii,kama unavyotegemea CCM itashinda ndivyo ninavyofahamu kwamba baada ya tare 31 october Dr Slaa ataapishwa, huo kwangu ndio ukweli kama ulivyo kwako tukubaliane kutofautiana
 
CCM ina wanachama mil 4 anavyosema Makamba. Tuliojiandikisha kupiga kura ni mil 19 anavyosema Kiravu.
Hao mil 4 wote watampa kura JK?
Jibu unalo: Ulichotakiwa kusema mtaji mkubwa wa JK kushinda uchaguzi ni Kuvuruga uchaguzi kupitia dola na kuiba kura we ni Tambwe Hiza?.
 

mimi ni mwanachama tangu mwaka 2000, amesahau kina SHIBUDA, MPENDAZOE na wengine wengi waliojeruhiwa CCM wameondoka na umati mkubwa japo kadi zao bado ni za CCM
 

Interesting............
 

Nadhani kosa lako kubwa ni kule kuamini kuwa kila mwamchama wa CCM ataipigia CCM. Unasahau kuwa hata mwanzilishi wa CCM Nyerere mwenyewe aliwahi kumpigia mgombea wa NCCR-Mageuzi akimwacha yule wa CCM. Kuna wana CCM wengi ambao watapenda kuona utawala ulioko madarakani unang'oka, siwezi kutaja majina yote ila watu kama Melecela na wafuasi wake, Salim na wafuasi wake, Bashe na wafuasi wake, akina Sabodo na akina Lwaitama.

Pili, unakosea tena kudhani kuwa watu wa vijijini bado ni wajinga kama zamani ambapo walikuwa ni blind loyals wa CCM. leo hii wameamka usingizini na ndio wa kwanza kuwazomea viongozi wa CCM huko vijijini. Inategemea uko sehemu zipi za nchi.
 
:smash:


Kuzunguka kwako sio sababu ya kutupa habari za kubahatisha, kwani umezunguka kufanya utafiti au kwa shughuli zako mwenyewe mkuu.. Mi nadhani Chadema wana wagombea ubunge na Madiwani sehemu nyingi sana kwenye hii nchi na wengi kati ya hao wamehama kutoka CCM, na mara ngapi tunaskia kwenye kampeni wanaCCM wanakataa baadhi ya wagombea wa hicho chama kwa sababu wamechaguliwa bila matakwa yao (wananchi) nenda kama umezunguka kweli najua hao utakua umewaona wengi tu, Wananchi wa karne hii sio wa kuwazungumzia kijuu juu tu namna hiyo, Halafu unasema vijana wengi wanakaa vijijin una uhakika lakin.. tupe link yenye hizo taarifa maana mi nachofahamu kutokana na hali ya uchumi kuwa tete vijana ndo wanaongoza kukimbilia mijini' siku hizi hata morani wamejaa mijini' Hayo makundi uliyotaja ni kama ya kufikirika hivi maana naona wanawake umewajumuisha, Kina Halima Mdee sijui umewajumlisha humo na wanawake wengi tu walioko Chadema!

Nadhani mtaji mkubwa wa CCM ni watu kama wew ambao bado wanaamini kwamba CCM ni POPULAR na ina wanachama wengi inasahau wanachama wa CCM wenyewe wengi ni km Lwaitama, na wengi wanazidi kukimbia.. kwani nani anautaka ufisadi kwa mfano wakati ye hana ata senti mfukoni!! Kama wana mtaji wangekua wanahangaika kwenda kudisrupt kampeni za wenzao na kupiga watu mabomu ya machozi km walivofanya Mwanza.. CCM wanajua hali tete, km walikua na mtaji basi wamechezea karata tatu, kurudi ni ndoto!! Wazee wenyewe siku hiz wamewachoka kwani unafkiri hawajawaona wenzao wakimwagiwa maji ya upupu' Maneno yako ni "speculations" ni kama unazungumzia hisia zako kuhusu demu umpendaye.. ni hayo tu!!
 
nafkiri KANU iliangushwa na muungano wa vyama! na tanzania chadema walilleta ubinafsi.. wametangaza mgo mbea wao late! alafu wakahitaji waungwe mkono na vyama vingine! .. "umoja ni nguvu utengano ni dhaifu!.. "
 
Hivi wengi wa watu kwenye mkutano wa Dr Slaa ni wingi wa kura zake? People hebu tukue kumbuka hii nchi haina middle class hivyo chochote ni inshalaah hebu tuache hizi hadithi za alinacho. Watanzania kuanzia wa vijijini ndo wana haki nani awe raisi siyo MM wala wala sauti ya umeme
 
Sauti ya umeme ni hanisi mmoja ambaye amekuwa akitegemea baba yake ampe yaliyotokea kamati kuu ndani na atuletea. Hawa ni looser wakati wao umepitwa hawana nafasi tena ya kuwakoga wagogoi, after all msiye mjua huyu FEM ni mtoto wa nyumba ndogo hivyo awe na adabu kwa ndugu zake.
 

Mbona kwa CCM umesahau wizi wa kura, kutumia katiba isiyojali demokrasia mfano ibara ya 41 (7), kutumia dola au nguvu, kutumia vitisho?
 
Mkuu mimi na wewe tunaweza kukubaliana kutokubaliana kwetu kwa maana ya nani anasera nzuri, lakini swala la hali halisi ya kitu niswala lingine, kunaweza kukawa na hitaji la mageuzi lakini mageuzi yana misingi yake ambayo ni lazima itimizwe ili kuleta hayo mageuzi,na si swala la kudhani muda umefika bila kuuandaa muda huo.
dhana ya kila anaye kwenda mashindanoni anategemea kushinda ni kweli ipo, lakini tusisahau pia hali halisi na nguvu ya kila mshindani, wakati mwingine kuna washindani ili washinde inaitajika zaidi ya miujiza kushinda,ingawa watajipa moyo kushinda


mimi ni mwanachama tangu mwaka 2000, amesahau kina SHIBUDA, MPENDAZOE na wengine wengi waliojeruhiwa CCM wameondoka na umati mkubwa japo kadi zao bado ni za CCM

Mbona wote mnakimbilia hili la wanachama tu, makundi mengine hamuyaoni? mimi nawahakikishia wapo wanachama CCM wa ukweli achana na hao akina nani ambao ni maarufu, wapo tunaishi nao mitaani, hata ukipunguza vipi lakini mtaji huu bado upo,
Unajua watu tunajidanganya na vitu visivyo na mantiki, Kwamfano ukiangalia kwa haraka haraka mkutano wa JK karatu jana, ule umati unaweza kudhani CCM itashinda jimbo hilo, ila ukweli ni kuwa jimbo lile ni la Slaa kwamaana ya CHADEMA na mgombea wao
 
Ni kweli kuwa CCM ina wananchama wengi kuliko hata wananchama wa vyama vingine vyote vya siasa. Ni kweli pia kuwa, kuna waTanzania wengi sana ambao hawana uanachama wa chama chochote cha siasa. Watanzania wasio na usajili wa chama chochote, ni wengi zaidi ukilinganisha na wananchama walijisajili kwenye vyama vya siasa nchini. Ni rahisi kupata uthibitisho huu kutokana na idadi ya wanachama wa CCM.

Pamoja na mtaji huu wa CCM, kuna wananchama ndani ya CCM ambao hawana imani na baadhi ya viongozi wa juu wa chama hicho, na hasa mgombea wao wa urais. Vile vile, kuna wananchama wengi tu wa CCM ambao hawakuridhishwa na utaratibu wa uchaguzi wa kura za maoni na hivyo wanahisi kuonewa kwa kunyang'anywa ushindi. Hawa wana mashabiki wao ambao wanaweza kuidhuru sana CCM katika uchaguzi huu (rejea: Kura za maruhani ambazo ni maarufu sana CCM).


Ni kweli pia kuwa Wazee wengi bado wana imani na CCM na wanaweza kuichagua. Ni vigumu kujua kwa usahihi kundi hili lina watu wangapi na uwezo wao wa kubadili matokeo ni mkubwa kiasi gani. Nimeshukudia pia baadhi ya wazee wakimshabikia Dr. Slaa na Prof. Lipumba.

Kama una uwezo wa kuonyesha idadi au kiwango cha ushawishi wa wazee ku-support hoja yako, itakuwa vizuri sana.

Katika kipindi kibaya kabisa cha ushiriki wa wanawake, ni hiki cha mwaka 2010. Idadi kubwa sana ya wanawake na vijana imejiandikisha kupiga kura. Inawezekana wakapigia CCM au chama kingine chochote. Ila nijuavyo ni kwamba, kama waume za wanawake hao wakiweka msimamo na kuongeza ushawishi kwa wanawake hao juu ya uchaguzi wa mgombea, basi maajabu makubwa ziadi yanaweza kutokea. Maana wanawake wengi husikiliza sana waume zao. Hapa nazungumzia wanawake wa umri wa kati na wazee.

Hili ni kweli kabisa. Ila linategemea sana influence ya ndugu zao wa mijini. Siku hizi simu za mkononi ambazo huduma zake zinafika hadi vijijini, zinabadili sana kundi hili na kulifanya liwe na ufahamu mkubwa zaidi kuliko miaka ya nyuma.

Tusubiri tuone nini kitakachotokea vijijini wakati huu.

Kwa upande wa CHADEMA sitakuwa na mengi sana ya kuandika sababu napata shida kidogo kupata hasa mtajiwao ukowapi, kama nitakuwa sivyo nahakika wadau mtanisawazisha
Ni kwlei kuwa katika majimbo ambayo CCM imeshajitwalia hata kabla ya uchaguzi, yanaonyesha kuwa na nafasi kubwa ya kuchagua Rais na wagombea ambao hawajapita bila kupingwa kutoka CCM. Lakini inawezekana pia kuwa baadhi ya waliopita bila kupingwa walitumia ulaghai na kuweza kuachiwa nafasi na wagombea wa upinzani kama ilivyoonekana katika baadhi ya majimbo. Kama hili ni kweli, itakuwa vigumu sana kuwa na uhakika kuwa wagombea watakaochaguliwa kutoka huko watashinda kwa kiasi kikubwa sana.

Nadhani kuna mengi tutakayojifunza baada ya kuisha kwa uchaguzi huu. Kikubwa ninachokiona, ni funzo la uhakika wa yanayosemwa na yanayotendwa na wananchi katika kuamua mustakbali wao. Bado siku chache sana. Tusubiri, tutaona.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…