Kabla ya kulalamika hapatikani, Je wewe unapatikana?

Kidagaa kimemwozea

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2018
Posts
3,680
Reaction score
6,554
Kabla ya kulalamika ni vigumu kumpata mtu fulani, je wewe watu wanakupata wanapokuwa wanakuhitaji kulingana na majukumu uliyopewa? Ukipigiwa simu unapokea? Ukitumiwa ujumbe WhatsApp unajibu?

Wengi wenu ni vigumu kupatikana kwasababu mnajiweka kwenye standard za juu bila kuzingatia majukumu. Ikifika siku na wewe unatafuta mtu fulani hapatikani na wewe unaanza kulalamika
 
Waziri pekee anayetumikia wananchi ni Gwajima anapokea cm na anajibu jumbe, haya mengine ni matapeli tupu
 
Watu wengi wanaojifanya hawapatikani kwenye taasisi za umma ni incompetent na sio wawajibikaji.

Wanajifichia kwenye kichaka cha kutokupatikana.
 
Viongozi wengine nchi yetu ni NGUMU mno kuwapata. Mimi Kuna kiongozi wa kitaifa Nina miezi 11 nimeomba nafasi ya kuonana naye Hadi leo holaa. "Eeh MUNGU ione nchi yetu hii."
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…