Parabolic
JF-Expert Member
- Dec 3, 2013
- 2,580
- 1,987
Tangu Chama cha Demokrasia na Maendeleo kilipotangaza kauli mbiu yake ya No reforms No Election ikimaanisha hakuna mabadililiko hakuna uchaguzi, kumekuwa na maoni tofauti ya utekekelezaji wa kauli mbiu hiyo.
Baada ya uongozi mpya kuingia chini ya Tundu Lissu, msisitizo umekuwa sio tu kususia uchaguzi, bali watauzuia usifanyike. Kauli hiii ndio imeongeza sintofahamu kwamba, Chadema wana uwezo gani wa kuzuia uchaguzi usifanyike?
Ni sawa na chura kumzuia tembo asinywe maji mtoni, maana yake hapo chura atapiga kelele halafu tembo atakuja kunywa maji halafu akiondoka, chura ataendelea kupiga kelele.
Swali hilo kwamba Chadema itazuia uchaguzi ni kwa msingi kwamba, CCM sio chama cha siasa tu, bali ni chama Dola. Mwenyekiti wake ni Rais wa Jamhuri ya Muungano na ana mamlaka makubwa kwa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, ana mamlaka vyombo vyote vya Serikali. Hata hiyo Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi ana mamlaka nayo, kwani uongozi wake ni lazima upate Baraka za Rais.
Sasa kwa mazingira hayop uchaguzi utazuiwaje? Je, Chadema itaitisha maandamano nchi nzima kupinga uchaguzi usifanyike? Je, watawashawishi wananchi wengi wasusie uchaguzi? Watakubali?
Kuna kila dalili kwamba CCM hawako tayari kuwasikiliza Chadema kwa namna yaoyote. Tumemsikia Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM, Amos Makalla akikejeli kkauli za Chadema, huku akisisitiza kuwa kama ni mabadiliko tayari yameshafanyika.
Makalla amezungumzia mabadiliko ya Kisheria yaliyoiunga Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, mabadiliko ya Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani na Mabadiliko ya Sheria ya Vyama vya siasa, akisema yamezingatia yaliyokuwa malalamiko ya wapinzani katika chaguzi.
Hata hivyo, Chadema wanapinga wakitupilia mbali mabadiliko hayo wakisema ni danganya toto.
Pia soma: Pre GE2025 - Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
Pamoja na ukweli kwamba, Chadema hawana nguvu za Dola kuzuia uchaguzi na wala wanaweza wasiwe na ushawishi wa kutosha kushinikiza mabadiliko wanayotaka, lakini hoja zao ni za msingi.
Wakati CCM wakisema kuwa kama ni mabadiliko yameshafanyika, lakini ushahidi wa wazi kwamba hakuna mabadiliko yoyote ni uchaguzi tu wa Serikali za Mitaa wa Novemba 2024, ambapo uonevu wa wazi wazi umeonekana.
Zaidi ya asilimia 60 ya wagombea wa upinzani hususani Chadema, ACT na vyama vingine walienguliwa bila sababu za msingi. Maana yake, CCM iliingia kwenye uchaguzi ikiwa na zaidi ya asilimia 60 ya wagombea wasio na wapinzani. Hata kile kinachoelezwa kwamba wagombea hawatapita bila kupingwa kimekuwa ni kiini macho tu.
Hapo ndipo unaposikia CCM imeshinda kwa asilimia 98, maana yake hapo Zaidi ya asilimia 60 ya wagombea walipita bila kuchaguliwa na wananchi ila ni kwa mizengwe ya kuenguliwa wapinzani.
Ushahidi wa pili ni kauli za viongozi wa Serikali na CCM. Tunakumbuka kauli ya aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Longodo (Arusha), Marco Ng'umbi aliyeeleza yaliyofanyika katika uchaguzi mkuu wa 2020. Alisema katika wilaya hiyo hakuna diwani aliyepita kwa kufanya kampeni bali ni kwa nguvu za Serikali. Alisema ni mazingira yaliyotengenezwa na Serikali na ndiyo inayofanya kazi hiyo kuhakikisha wagombea wa CCM kushinda.
Ni kweli Ng’umbi alitenguliwa uteuzi wake, lakini ukweli ndio huo unaofanyika nyuma ya pazia.
Tumesikia pia kauli za Mbunge wa Mtama akieleza kwamba ushindi haupatikani tu kwenye sanduku la kura. Nape huyo huyo alishawahi kunukuliwa akisema kuwa CCM itashinda hata kwa goli la mkono. Unafikiri hizo kauli ni za bahati mbaya? Hata kama ametenguliwa uwaziri, amepewa adhabu gani, lakini huo ndio ukweli unaotekelezwa.
Kilichofanywa kwenye mabadiliko ya Sheria za Uchaguzi ni kupakapaka mafuta lakini sharia bado ni mbovu vilevile. Halafu Rais Samia ambaye ndiye mgombea wa CCM bado anahusika katika kupatikana kwa viongozi wa inayoitwa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, kwa mujibu wa Sheria ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi Kifungu cha 4(1 na 2).
Vilevile Rais ndiye mtumishi namba moja wa Serikali yaani anasimamia watumishi wote. Leo hata kama Wakurugenzi wa halmashauri hawasimamii uchaguzi, bado watumishi wa Serikali wanaowajibika kwa Rais ndio watasimamia. Hausimamiwi tu na Tume
Maana yake mgombea wa CCM ana mamlaka na wasimamizi wa uchaguzi. Hapo kuna uchaguzi gani huru utafanyika?
Uchaguzi hausimamiwi tu na tume, bali pia kuna vyombo vya Dola, kuna majeshi ya ulinzi na usalama yanayowajibika kwa Rais, kuna wakuu wa mikoa na wilaya kote huko wana mamlaka kwa njia moja au nyingine katika uchaguzi.
Hapo tena kura haiakisi nguvu ya mwananchi, bali mamlaka ya Dola ndio itakayoamua nani ashinde au nani asishinde.
Sasa kabla ya kukimbilia kuhoji, Chadema watazuiaje uchaguzi, tujiulize, uchaguzi wa aina hii unafanyikaje? Je, Chadema wakubali kuingia kichwakichwa wachinjwe au wabariki mchakato ovu?
Kuna uwezekano mkubwa wa baadhi ya vyama vya siasa vikashiriki uchaguzi huo na vikaipinga Chadema. Kuna uwezekano pia kama alivyosema Makalla, Chadema isiposhiriki uchaguzi kitapoteza nafasi ya kuwa chama kikuu cha upinzani. Maana yake kitatafutwa chama mbadala ili kionekane ndio kina nguvu na kimeshiriki uchaguzi na kimeridhia matokeo hata yawe mabaya kiasi gani.
Iwe iwavyo, Chadema washiriki uchaguzi au wasishiriki, lakini la msingi ni ukweli wa hoja zao, hapo ndipo mjadala ujikite.
Wengine wanasema kuna wagombea wengi wa Chadema wa ubunge na udiwani, ndio watakuwa wamepoteza chama hicho kisiposhiriki uchaguzi? Lakini swali linabaki pale pale, kwamba wanakwenda kushiriki kwenye uchaguzi kama huo wa Serikali za Mitaa Novemba 2024?
Ni wakati sasa kujadili mfumo wetu wa uchaguzi na kuamua hatma ya demokrasia yetu.