Kabla ya kuzoeana!

Kabla ya kuzoeana!

Mkwaruzo

JF-Expert Member
Joined
Feb 21, 2011
Posts
563
Reaction score
98
Mambo kama ujumbe mfupi wa kuambiana nakupenda, unafanya nini sahizi, karibu tule. Ni maneno ambayo wapenzi huyapenda sana lakini wakizoeana ...mh...
SIJUWI!
Mambo kama haya hukatisha sana tamaa yanapotokea kwa hafla kama huamini JARIBU
 
Kipi kitafua? Ndiyo hofu yangu inayonifanya nisitake kuhakisha hili
 
Kwa hiyo wewe mwenzetu uko kwenye stage ya kuambiwa " karibu tule" au unataka kutuambia nini ulipoanzisha hii thread?
 
Mambo kama ujumbe mfupi wa kuambiana nakupenda, unafanya nini sahizi, karibu tule. Ni maneno ambayo wapenzi huyapenda sana lakini wakizoeana ...mh...
SIJUWI!
Mambo kama haya hukatisha sana tamaa yanapotokea kwa hafla kama huamini JARIBU[/QUOT

nafikiri hayo maneno yamekaa kizanzibar zaidi,....
 
Kwa hiyo wewe mwenzetu uko kwenye stage ya kuambiwa " karibu tule" au unataka kutuambia nini ulipoanzisha hii thread?

hata kama sipo ktk stage hiyo lkn sitoweza kuiruka pale nitakapoamua kuingia ktk uhusiano (mpya). Ww kama una data zozote weka....
 
Ulikuwa hujui eehhh?? Yanakwisha tena hata mpenzi ni issue kutolewa hilo neno.

Tafuta thread moja iliwahi kuanzishwa kuhusu hilo
 
Mbona wapo wanaoendelea hivyo hivyo!Tatizo ni kwamba wengi wakishapata na wakishazoeana wanadhani hamna tena haja yakuonyeshana mapenzi na kujaliana wakiwa mbali mbali!!
 
Kabla ya kuzoeana, kila mmoja hujaribu kumfanyia mambo kede kede mwenzake ili kumfurahisha na kuonyesha ni jinsi gani anavyomjali na kumthamini. Mambo huendelea hivyo hivyo hadi kufikia hatua ya kuzoeana. Hapo kila mmoja anakua anajua kipi mwenzake anapenda na nini hapendi. Hapo panakuwa na fursa ya kusamarize yale mengi mliyokuwa mnafanyiana awali kwa kumfanyia yale tu anayoyapenda. Lakini mambo yanakuwa kinyume chake kwani hata hayo machache inakuwa ni tabu kuyapa muendelezo kama ilivyokuwa mwanzoni. Hali husababishwa na nini hasa??
 
Hivi kuna qualification ya age kuingia JF,kama haipo inabidi ianzishwe mapema sana
 
Kwenye LOVE kuna stage mbalimbali,

KUCHOKOZANA:
Kipindi cha kuhakikisha unamdaka mwenzio vizuri ili muingie vizuri kwenye laini mara nyingi kunajawa na vituko vya kumfurahisha mwenzi.

MAPENZI MOTOMOTO:
Mapenzi motomoto kila saa unataka muwe pamoja kwa kila hali na mali hata bafuni mnataka kuogeshana pamoja

MAPENZI TABIA:
Hiki ni kipindi cha kuanza kuonesha tabia za mtu laivu kwa mwenzi

MAPENZI MAELEWANO:
Hapa ndo kila mtu anaelewana na mwenzi kwa kila hatua kuanzia kwenye mawasiliano, ratiba, hobby na hulka mbalimbali

MAPENZI KICHOVU:
Hiki ni kipindi ambacho kila mtu anaona kama mwenzi ni mzigo na ni kipindi hasa cha majaribu inafika mahali unajiuliza hivi kweli huyu ni mwenzi wangu wa ukweli ama la?

MAPENZI MAJIBU:
Ni kipindi ambacho ukienda kwa mwingine utaona huyo mpya hajamfikia mpenzi wako kwa level fulani hasa kwenye kucare, busara, uchaji wa Mungu, tabia, response mbalimbali, kero na mengineyo mengi na kipindi ambacho mtu anatoa maamuzi ya kuwa HUYU NDIYE WANGU HASWA!!
 
Hivi kuna qualification ya age kuingia JF,kama haipo inabidi ianzishwe mapema sana

Kama vipi, tujiunge jf kwa kutumia vyeti vya kuzaliwa baada ya kupendekeza huo umri unaona unafaa. Sikiliza broo, ubora wa kutaka kujuwa kitu, ni kujifunza kabla hujakiingia. Kitu chengine, kama umeona nimekosea kuweka thread, ww ni bora unielekeze tu na siyo kunirudisha nyuma kimawazo kwa kuhoji vitu tofauti. Kinachoweza kupatikana kupitia mm, na ww kinaweza kukufaa pia.
 
Kwenye LOVE kuna stage mbalimbali,

KUCHOKOZANA:
Kipindi cha kuhakikisha unamdaka mwenzio vizuri ili muingie vizuri kwenye laini mara nyingi kunajawa na vituko vya kumfurahisha mwenzi.

MAPENZI MOTOMOTO:
Mapenzi motomoto kila saa unataka muwe pamoja kwa kila hali na mali hata bafuni mnataka kuogeshana pamoja

MAPENZI TABIA:
Hiki ni kipindi cha kuanza kuonesha tabia za mtu laivu kwa mwenzi

MAPENZI MAELEWANO:
Hapa ndo kila mtu anaelewana na mwenzi kwa kila hatua kuanzia kwenye mawasiliano, ratiba, hobby na hulka mbalimbali

MAPENZI KICHOVU:
Hiki ni kipindi ambacho kila mtu anaona kama mwenzi ni mzigo na ni kipindi hasa cha majaribu inafika mahali unajiuliza hivi kweli huyu ni mwenzi wangu wa ukweli ama la?

MAPENZI MAJIBU:
Ni kipindi ambacho ukienda kwa mwingine utaona huyo mpya hajamfikia mpenzi wako kwa level fulani hasa kwenye kucare, busara, uchaji wa Mungu, tabia, response mbalimbali, kero na mengineyo mengi na kipindi ambacho mtu anatoa maamuzi ya kuwa HUYU NDIYE WANGU HASWA!!

Now kuna vitu nimevijua. Asante kwa uchambuzi wako.
 
Mambo kama ujumbe mfupi wa kuambiana nakupenda, unafanya nini sahizi, karibu tule. Ni maneno ambayo wapenzi huyapenda sana lakini wakizoeana ...mh...
SIJUWI!
Mambo kama haya hukatisha sana tamaa yanapotokea kwa hafla kama huamini JARIBU

tumezoeana mwaka wa 74 sasa ila bado tunauliza..
.
 
Now kuna vitu nimevijua. Asante kwa uchambuzi wako.

Mkwaruzo,

Ndo hivyo, yaani LOVE ina stage mbalimbali lazima mpitie, tofauti inajitokeza katika stage moja wapo mpaka unafikia mnatofautiana na mnaamua kuachana, mara nyingi inatokea hasa kwenye Stage za Mapenzi tabia, Mapenzi maelewano, Mapenzi kichovu na Majibu.

Tupo pamoja mkuu!
 
Yote hayo huja unapoelewa luv ni part ya maisha hivyo kuna curriculum yake na hivyo vijineno ni sehemu ya contents of luv at its consistence.
 
Back
Top Bottom