Kwenye LOVE kuna stage mbalimbali,
KUCHOKOZANA:
Kipindi cha kuhakikisha unamdaka mwenzio vizuri ili muingie vizuri kwenye laini mara nyingi kunajawa na vituko vya kumfurahisha mwenzi.
MAPENZI MOTOMOTO:
Mapenzi motomoto kila saa unataka muwe pamoja kwa kila hali na mali hata bafuni mnataka kuogeshana pamoja
MAPENZI TABIA:
Hiki ni kipindi cha kuanza kuonesha tabia za mtu laivu kwa mwenzi
MAPENZI MAELEWANO:
Hapa ndo kila mtu anaelewana na mwenzi kwa kila hatua kuanzia kwenye mawasiliano, ratiba, hobby na hulka mbalimbali
MAPENZI KICHOVU:
Hiki ni kipindi ambacho kila mtu anaona kama mwenzi ni mzigo na ni kipindi hasa cha majaribu inafika mahali unajiuliza hivi kweli huyu ni mwenzi wangu wa ukweli ama la?
MAPENZI MAJIBU:
Ni kipindi ambacho ukienda kwa mwingine utaona huyo mpya hajamfikia mpenzi wako kwa level fulani hasa kwenye kucare, busara, uchaji wa Mungu, tabia, response mbalimbali, kero na mengineyo mengi na kipindi ambacho mtu anatoa maamuzi ya kuwa HUYU NDIYE WANGU HASWA!!