MGOGOHALISI
JF-Expert Member
- Apr 16, 2011
- 3,294
- 4,920
Hii tunarudia kumwambia raisi Samia na washauri wake (ambao katika hili sioni kama walimshauri) kuwa kama ulishaamua kuwatema hawa watu basi endelea na msimamo wako. Ni hiari ya raisi kuteua na kutengua wala halazimishwi. Ila inapotokea kelele za nje kuonekana tishio kwa maamuzi yake asitumie pesa za umma kuzima hizo kelele.
Serikali ina mifumo rasmi ya kazi na kuajiri. Kama raisi alishaona Kabudi na Wengine hawafai kuendelea nae angewaacha tu kwa sababu ile ile aliyoisema hadharani.
Lakini sasa tunawaona hawa watu wakiendelea kutumia mali ya umma huku nafasi zao zikiwa hazieleweki serikalini. Haya ni matumizi mabaya ya kodi za wananchi. Sio lazima Kabudi na Lukuvi waendelee kuwepo viunga vya ikulu. Kwanza ni wabunge wenye majimbo yao. Wanaweza kuendelea kuwatumikia wananchi huko majimboni.
Huu usemi wa kusema eti una kazi maalumu wakati sababu ya kubadili baraza ilishajulikani isiwe sababu ya kutumia kodi zetu vibaya. Namaliza kwa kusema Lukuvi na Kabudi sio lazima waendelee kuwepo viunga vya ikulu. Ni matumizi mabaya ya kodi za wananchi, ni kuwapotezea muda kutumika majimboni kwao.