Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
Hapo chini ni picha ya kaburi la Dossa Aziz lililopo kwenye hodhi ya familia yao Mtoni Kwa Aziz Ally.
Kuna kisa cha kusikitisha sana na siku hii ya mkasa wa Dossa na kwa hakika ni mkasa wa wazalendo wote.
Naikumbuka siku hii kwa kuwa ilitangazwa kuwa Mwalimu Nyerere atatoa nishani kwa Watanzania ambao wametoa mchango mkubwa kwa taifa.
Sherehe za kutunuku zilipoanza mimi nilikuwa na Abbas Mtemvu ndani ya gari yake tunatoka Kariakoo tunarejea makwetu Masaki.
Mimi siku ile mwaka wa 1985 nilikuwa na hakika kuwa Abdul Sykes na wazalendo wengine waliokuwa na Nyerere wakati wa kupigania uhuru watatunukiwa nishani na nikawa nasikiliza kwa makini ile sherehe ilivyokuwa inakwenda katika Viwanja Vya Ikulu.
Hakuna yeyote katika hawa wazalendo ambao wasomaji wangu mmekuwa mkiwasoma kwangu aliyetunikiwa nishani siku ile.
Katika kitabu cha Abdul Sykes nilikuja kuandika maneno hayo hapo chini:
''Tarehe 27 Aprili, 1985 Julius Kambarage Nyerere, sasa akijulikana kama Baba wa Taifa, katika sherehe kubwa katika Viwanja Vya Ikulu, alitoa jumla ya medali 3979 kwa Watanzania waliochangia katika maendeleo ya taifa.
Kati ya wale ambao walipewa medali hizo alikuwa Sheikh Abdallah Chaurembo.
Wazalendo waliotajwa ndani ya kitabu hiki ambao walipigania uhuru wa Tanganyika, hakuna hata mmoja wao aliyekuwa katika orodha ile ya heshima.
Moyo uliniuma sana.
Baada ya siku chache kupita, Nyerere kama mtu aliyegutuka alimualika Dossa Aziz Ikulu.
Dossa Aziz, wakati wa kudai uhuru wa Tanganyika alikuwa mtu maarufu, mwenye nafasi, na kujiweza sana.
Sasa Dossa baada ya miaka kupita hakuwa akifahamika tena na ule umaarufu na utajiri wake ulikuwa umetoweka.
Alikuwa akiishi maisha ya kawaida kijijini Mlandizi, maili chache nje ya Dar es Salaam.
Katika sherehe ya faragha Nyerere alimtunukia medali Dossa Aziz, rafiki yake wa zamani.''
Picha hiyo hapo chini Dossa Aziz akipewa medali na Mwalimu akiwa peke yake Ikulu.