Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
KABURI LA TEWA SAID TEWA MAKABURI YA MWINYIMKUU MAGOMENI
Tewa Said Tewa kwake nililokuwa mtoto wake mwanae kabisa.
Mzee Tewa Said Tewa akijuana na baba yangu toka udogoni na ujana wao.
Mzee Tewa akaniamini kama baba anavyomwamini mwanae.
Mzee Tewa alipojua naandika kitabu cha historia ya uhuru wa Tanganyika alinieleza mengi ambayo asingeweza kumweleza yeyote yule.
Siku zile watu waliishi kwa hofu wasingeweza hata kukuambia kuwa chanzo cha harakati za kuunda TANU na kudai uhuru wa Tanganyika si Julius Nyerere.
Tewa ndiye aliyenieleza kuwa katiba ya TANU haikuandikwa na Nyerere bali walinakili.kutoka katiba ya Convetions People's Party (CPP) ya Kwame Nkrumah wa Ghana.
Tewa ni kati ya watu waliomuona Nyerere alipofika mjini Dar es Salaam akienda kwa Abdul Sykes ambae nyumba yake haikuwa mbali na kwake pale Mtaa wa Stanley.
Hivi ndivyo alivyojuana na Nyerere wakawa wote ndani ya TAA kisha pamoja wakawa kati ya waasisi 17 waliounda TANU.
Tewa alinieleza maneno ambayo Abdul Sykes alimweleza usiku wa kuamkia uchaguzi wa TAA uliofanyika Arnautoglo Hall walipokubaliana kumchagua Nyerere kuwa President wa TAA April 1953 na mwaka unaofuatia waunde chama cha TANU.
Tewa aliniambia kuwa Abdul alimwambia kuwa wakishampa Nyerere chama hawataweza kumnyang'anya.
Alipofariki Mzee Tewa mwaka wa 1998 sikuwapo nchini na nilirejea muda mfupi baada ya kifo chake.
Nilishangaa kukuta kuwa, Tewa Said Tewa, Dossa Aziz na Zuberi Mtemvu wote vifo vyao vilikuwa vimepishana kwa muda mfupi sana usiozidi mwezi mmoja.
Niliangalia magazeti ya nyuma kutazama wahariri wamechapa nini kuhusu wazalendo wapigania uhuru hawa katika magazeti yao.
Hapakuwa na kitu.
Hawa wote watatu ni wazee wangu na wote nilipata kuzungumzanao kuhusu Julius Nyerere, historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika.
Picha ya mwisho ni safari ya Hijja mwaka wa 1964 Tewa Said Tewa akiwa na Abdul Sykes na Chief Abdallah Said Fundikira na watu wengine.
Namuomba Allah awaghufirie madhambi yao na awaingize Firdaus.
Amin.