Kaburi lafukuliwa Mbeya, mwili wanyofolewa viungo

Kaburi lafukuliwa Mbeya, mwili wanyofolewa viungo

Sildenafil Citrate

JF-Expert Member
Joined
Jan 29, 2021
Posts
577
Reaction score
2,595
Jeshi la Polisi Mkoani Mbeya linawasaka watu waliohusika kufukua kaburi na kunyofoa baadhi ya viungo vya mwili wa Neema Enock (24) uliozikwa kwenye kaburi hilo wilayani Rungwe.

Akizungumza na Mwananchi leo Jumanne Novemba 8, 2022 Kamanda wa Polis Mkoa wa Mbeya, Benjamin Kuzaga amesema tukio hilo limetokea jana katika makaburi ya Kamasuru kijiji la Kilasi Halmashauri ya Busokelo wilayani Rungwe.

Kamanda Kuzaga amesema baada ya kufukuliwa kaburi hilo baadhi ya viungo vya mwili wa Neema vilinyofolewa vikiwamo moyo, figo, jicho, ulimi na titi moja huku sehemu ya tumbo ikiwa imechanwa.

Amesema taarifa za awali zimeeleza kuwa Neema alifariki dunia Novemba 5, 2022 katika hosptali ya rufaa kitengo cha wazazi Meta muda mfupi baada ya kujifungua na mazishi yakafanyika Jumapili Novemba 6, 2022.

“Jambo la kusikitisha Novemba 7 mwaka huu majira ya asubuhi polisi walipata taarifa kutoka kwa ndugu wa marehemu kuhusiana na mwili wa ndugu yao kufukuliwa na kisha baadhi ya viungo kunyofolewa na watu wasiojulikana ”amesema.

Kamanda Kuzaga amesema baada ya kupata taarifa waliambatana na madaktari mpaka makaburini ambapo walikuta mwili wa huo na walipofanya uchunguzi walibaini baadhi ha viungo vimenyofolewa.

Kamanda Kuzaga amesema chanzo cha tukio hilo ni imani za kishirikina.

Amesema kuwa Jeshi la Polisi linalaani tukio hilo na msako mkali unaendelea ndani na nje ya Mkoa wa Mbeya ili kubaini waliohusika.

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Juma Homera amesema Wilaya ya rungwe imekuwa kinara kwa matukio ya mauaji yanayohusisha imani za kishirikina.

“Nimeagiza Jeshi la Polisi kufanya opareshini kali kuhakikisha watuhumiwa wanakamatwa kwani kitendo kilichofanywa cha kunyofoa viungo vya binadamu ni cha kinyama na ukatili wa kijinsia” amesema.

Awali Mkuu wa Wilaya ya Rungwe, Dk Vicent Anney alifanya Mkutano na viongozi wa dini kukemea vitendo vya ukatili vinavyoendelea kutokea wilayani humo ikiwamo mauaji yanayohusishwa na imani za kishirikina.

Chanzo: Mwananchi
 
umaskini na tamaa ya pesa za haraka ndo vinachangia matukio kama hya kuendlea
kuwepo..
 
Hii dunia!!!!!!!
Kuna wakati unaweza kukosea kwa kujiuliza mambo mengi sana!!
 
Hii nchi tunakoelekea, ni mungu tu ndiye anayejua
 
Kuna mganga sasa hivi anatengeneza zindiko kutumia viungo vya marehemu
 
Tunahitaji sana Elimu ya Mabadiliko ya FIKRA KWA JAMII YETU.
Fikra Dumavu ndio chanzo cha matukio ya Ukatili kushamiri dhidi ya Jamii zetu[emoji848][emoji22]
 
Mbeya huwa wana matukio ambayo ukifikiria hayaingii akilini
 
Pamoja na makanisa yao yote bado wanafanya uasi kama huu, hakuna mkamilifu ila kwa haya yanayotokea tukichomwa jua na kukosa maji ni halali
 
Back
Top Bottom