Wana JF heshima zenu wakuu .
Leo baada ya kuona Ngeleja kaanza kutoa matamko ya kugawa Umeme Mbeya vijijini huku akijua kwamba kuna moto waja nimekumbuka juu ya Jimbo la Ndugu Pharacy Kabuye .Sijui nimepatia jina lake ama la lakini bado najiuliza kwa nini hadi leo NEC hawajaitisha uchaguzi ? Kuna shida gani na wanakwama wapi ? Maana najua hakuna rufaa iliyo katwa baada ya kutenguliwa .Je tunaweza kuona uchaguzi wa Mbeya vijijini haraka kuliko kule kwa Kabuye ? Naombeni mtizamo wenu wakuu .
This time wanataka kununua shahada zote kabla hajatangaza uchaguzi wa marudio maana tarime imekuwa fundisho.
Hivi vyama vya siasa haviwezi kuishitaki tume ya uchaguzi kwa kukiuka taratibu za uchaguzi?????? maana wananchi wa jimbo hilo wanakoseshwa haki yao ya kuwakilishwa na kusikilizwa maoni yao kupitia mbunge wao.
Nina imani si kazi ya Vyama kuitaka haki hii ila ni haki ya Watanzania wa Muleba kwenda Mahakamani na kufungua kesi ya kunyimwa haki .Shahada hawawezi kununua wakazimaliza .Mambo ya Tarime kama CCM yataka kuwajibu basi basi they must deliver na si kununua shahada .
Ni kweli vyama haviwezi kufanya hiyo kazi lakini nani atawaorganise hao watu???
Je kituo cha Demokrasia wamefanya nini kuhakikisha demokrasia ya watu wa Muleba imetimizwa??? Vyama vya vuguvugu (pressure groups) mko wapi????
Mwanasheria mkuu na other law enforcers mko wapi watu wanakosa haki yao ya msingi????
Nina imani si kazi ya Vyama kuitaka haki hii ila ni haki ya Watanzania wa Muleba kwenda Mahakamani na kufungua kesi ya kunyimwa haki .Shahada hawawezi kununua wakazimaliza .Mambo ya Tarime kama CCM yataka kuwajibu basi basi they must deliver na si kununua shahada .
Wana JF heshima zenu wakuu .
Leo baada ya kuona Ngeleja kaanza kutoa matamko ya kugawa Umeme Mbeya vijijini huku akijua kwamba kuna moto waja nimekumbuka juu ya Jimbo la Ndugu Pharacy Kabuye .Sijui nimepatia jina lake ama la lakini bado najiuliza kwa nini hadi leo NEC hawajaitisha uchaguzi ? Kuna shida gani na wanakwama wapi ? Maana najua hakuna rufaa iliyo katwa baada ya kutenguliwa .Je tunaweza kuona uchaguzi wa Mbeya vijijini haraka kuliko kule kwa Kabuye ? Naombeni mtizamo wenu wakuu .
Kabuye kakata rufaa kupinga maamuzi ya mahakama kuu sasa mnataka uchaguzi ufanyike kivipi?
Get organised before being carried away sons.....
Wakuu sinasikia kua kuna sheria inayozuia uchaguzi mdogo, mika miwili kabla ya uchaguzi mkuu, au?
Maana bada ya Tarime, niilmuuliza Mkulu mmoja wa CCM aliyekua huko Tarime, kwamba vipi Mwibara na Biharamulo, akaniambia kwamba ukifanyika sasa hivi CCM itakula hewa, lakini haiwezi kufanyika miaka miwili kabla ya general elections kwa hiyo haitkuwepo, Mkuu Lunyungu vipi imekaaje hii?
Naomba kuuliza Kabuye ni yule mbunge aliyetoa mfano wa wabunge wengine wako kama kuku kulala hapohapo na wanakunya hapohapo?