Kabwili awasha moto Simba, TFF

Kabwili awasha moto Simba, TFF

Suley2019

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2019
Posts
2,203
Reaction score
5,610
1580277536114.png

Kabwili alitoa kauli hiyo wakati akizungumza na kituo kimoja cha redio nchini, ambapo alieleza kuwa Simba ilimshawishi afanye kosa kwenye mechi dhidi ya JKT Tanzania litakalomfanya aonyeshwe kadi ya njano na kufikisha idadi ya kadi zitakazomsababisha akose mechi iliyofuata baina ya watani wa jadi msimu uliopita.

Hata hivyo, Kabwili aliyesimama langoni kwenye mechi dhidi ya Simba Februari 16, mwaka jana, Yanga ikichapwa 1-0, kwa bao pekee la mshambuliaji Mnyarwanda Meddie Kagere katika dakika ya 72, alisema hakukubali kushiriki mpango huo.

Tayari Shirikisho la Soka nchini (TFF), limeiagiza Kamati yake ya Maadili kufuatilia ukweli kuhusu tuhuma hizo za upangaji matokeo zilizotolewa na Kabwili.
Taarifa ya Ofisa Habari wa TFF, Clfford Ndimbo juzi ilieleza kwamba baada ya shirikisho kusikia tuhuma hizo zilizotolewa na Kabwili kupitia vyombo vya Habari, Sekretarieti imeiandikia barua Kamati yake ya Maadili kufanyia kazi suala hilo.

Aidha, TFF pia imeeleza itavijulisha vyombo vingine vya usalama ili visaidie uchunguzi na kuchukua hatua stahiki.

Hata hivyo, Klabu ya Simba jana ilionyesha kukerwa na kukasirishwa na kauli hiyo ya Kabwili, na katika taarifa yake, imeeleza: "Klabu ya Simba imepokea kwa masikitiko kauli ya mchezaji Ramadhani Kabwili aliyoitoa Januari 27, 2020.

"Kauli za aina hii kutoka kwa wachezaji ni za kuchukiza na sio za heshima ambazo zinaashiria upangaji wa matokeo ya mechi kama ilivyotuhumiwa na mchezaji huyu. Kauli ambazo Klabu ya Simba inazipinga na kukemea vikali."

Taarifa hiyo iliendelea kufafanua kuwa kauli kama hizo zina madhara makubwa kwenye uadilifu wa Klabu ya Simba na viongozi wake na kwamba uadilifu na heshima ya TFF kwa ujumla unawekwa mashakani kama kauli za namna hiyo hazitachukuliwa hatua kali.

"Klabu ya Simba inafurahishwa na hatua za haraka zilizochukuliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania dhidi ya kauli kama hizi kwa vyombo husika. Klabu ya Simba inaamini kwamba jambo hili liko mbele ya mikono ya vyombo husika na litachukuliwa hatua stahiki kwa haraka," iliongeza taarifa hiyo.

Kwa upande wa Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli, alisema wapo tayari kutoa ushirikiano watakaohitajika kuutoa kwa TFF na vyombo husika baada ya kuzungumza na Kabwili ili kukomesha vitendo kama hivyo vinavyozuia ukuaji wa soka la Tanzania.

Lakini pia, Bumbuli alikiri Kabwili kwenda kinyume na taratibu za klabu hiyo zinazozuia wachezaji wake kwenda kuongea moja kwa moja na vyombo vya habari pasipo ridhaa ya klabu.

IPP Media
 
Back
Top Bottom