St. Paka Mweusi
JF-Expert Member
- Sep 3, 2010
- 7,956
- 5,149
Dunia haiishi vya kushangaza,mwenzenu jana nimepata mgeni mtoto wa kijerumani,na kwa kuwa tulipanga anitembelee nikamwambia nitakupikia chakula cha kiafrika.Na kweli mtoto wa kiume nikapitia kwa mchina nikachukua utumbo wa mbuzi na ndizi matoke.Nikaandaa utumbo kwa ufundi wangu wote, nikaweka vitunguu swaumu,tangawizi,limao,pilipili mbuzi kwa mbali,kitunguu maji,nyanya ya kopo,pilipili hoho na mazagazaga kibao ya kiafrika.Mgeni wangu alipofika nikamkaribisha na alifurahia akasema tangu azaliwe hajawahi kula chakula kitamu kama hicho na ameniomba akanitambulishe kwa wazazi wake kama mchumba mwenye sifa ya upishi.Sasa wandugu naombeni ushauri nikubali kutambulishwa au huo ndio utakuwa mwanzo wa kugeuzwa hausi boi.