SoC03 Kachiru Shujaa wa Mtakuja Shule ya Msingi

SoC03 Kachiru Shujaa wa Mtakuja Shule ya Msingi

Stories of Change - 2023 Competition

Rupia Marko D

Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
39
Reaction score
63
KACHIRU SHUJAA WA MTAKUJA SHULE YA MSINGI.'
Mwanzo
...Ndugu msomaji karibu pamoja nami kwa faraja nikikusindikiza kusoma simulizi hii ya kuvutia ya Mwalimu Kachiru na mafanikio ya Shule ya Msingi Mtakuja, kua nami mwanzo mpaka mwisho.

Katika kijiji cha ujirani mwema aliishi mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Kachiru, kwa nyazifa alikuwa ni mwalimu mkuu katika shule ya msingi Mtakuja.

Basi kabla ya yeye kutunukiwa hiyo nyazifa kipindi akiwa tu ni mwalimu wa kawaida, tena mwalimu wa Jiografia na Sayansi kwa darasa la Saba. Shule ya Mtakuja ilikuwa ikifanya vibaya sana katika matokeo yake ya kata, wilaya pamoja na taifa kwa ujumla, kiasi kwamba iliwahi kushika mkia katika moja ya mitihini ya taifa.

Na si tu kitaaluma ambako ilifanya vibaya bali ni karibu katika kila nyanja nikimaanisha michezo na burudani, utunzaji mazingira, ushirikiano na shule jirani, nidhamu kwa walimu na wanafunzi haya ni miongoni mwa machache kati ya mengi yaliyochagiza shule hii ya Mtakuja kushindwa kufanya vema.

Hivyo basi hali hii ilipokua ivi Serikali ya mtaa ilingilia kati na kuona ni namna gani ya kuweza kunusuru maendeleo ya watoto wao kwa ustawi wao wa hapo badae, hii hali ikawafanya viongozi wa mtaa na baadhi ya wakereketwa kupeleka mashtaka katika ngazi ya juu yaani Wilayani hapo ndipo Serikali kupitia viongozi wakebwa manispaa walipoamua kuingilia kati na kumtumbua aliyekua mkuu wa kipindi hicho katika shule hiyo ya Mtakuja.

Na kama bahati njema ambavyo huwaangukia wote tena kama vile mvua iwanyesheavyo wote wabaya kwa wema, bahati hii ikamuangukia mwalimu Kachiru.

Ilikuwa ni siku ya jumapili Mwalimu Kachiru alivoteuliwa kua mwalimu mkuu mpya wa shule ya Mtakuja. Basi Siku zikaenda kama upepo uendavyo na wiki moja baada ya uteuzi huu matunda mema ya uongozi wake yakaanza kuonekana, ilikuwa ni asubuhi moja katika siku ya jumatatu, mda ambapo wanafunzi walikua wamekutanika wote pamoja assemble( mstarini) Mwalimu Mkuu Kachiru akasimama mbele na kuongea na wanafunzi wake kwa takribani masaa mawili miongoni mwa machache kati ya mengi aliyo yaongelea ni kua huku nikimnukuu alisema " wanangu wapendwa tulikua wazembe na ule uzembe wetu umetutafuna vya kutosha, basi tangu sasa na ifahamike miongoni mwenu nyote kua utaratibu wa masomo katika shule hii unabadirika na sote kwa pamoja hasa madarasa yaliyo katika mitihani tutasoma asubuhi na jioni, mimi kama mimi kwa nyazifa niliyopewa nitawashauri walimu wangu na sote kwa pamoja tutawandisha. Na juu ya yote adhabu kali itatolewa kwa wote wale watakao kiuka agizo langu, moja kati ya adhabu hizo ni adahabu ya kuruka kichura, kushika masikio kuiita mvua mpaka inyeshe isipo nyesha utashinda hapo siku nzima( wanafunzi wote wakacheka~ hahahah).

Basi zoezi hili likaanza wanafunzi wakawa wanarejea Shuleni kwa ajiri ya kujifunza zaidi na waliitikia kwa mwitikio mkubwa huku wakiogopa zile adhabu alizozitaja Mwalimu Mkuu Kachiru, mwalimu Kachiru alijitoa sana kukomesha watoro, hadi wanafunzi wakampa jina la SINDANO YA WATORO, walimuimba wakisema

Sindano hiyo inadunga,🎶
Sindano hiyo inachoma,🎼
Tena usipime inavouma,🎶
Mapele yote imedukua,🥁
Nayo majipu yametumbuka,🎼
Kachiru ni sindano yenye makali.🎺


Muda ukapepea kama upepo wa jangwani, wakati wa mitihani ukafika, wanafunzi wakaifanya kwa weredi mkubwa na matokeo yalipotoka watu walibaki midomo wazi kwa kua shule ya Mtakuja ilishika nafasi ya kwanza kiwilaya na nafasi ya kumi na moja kitaifa.

Kama ilivyo kawaida wanafunzi waliofanya vizuri waliitwa na kupewa zawadi na pia Mwalimu mkuu naye alipewa zawadi.

Juhudi zake pia hazikuishia hapa Mwalimu Mkuu Kachiru alihakikisha ustawi wa Mazingira kwa kupanda miti kuzunguka Shule huku yeye mwenyewe akishika jembe na kuonesha mfano dhahiri kwa kupanda miche ya miti mitano, na wanafunzi nao wakapanda miche ya miti na shule yao ikapendeza sanaa.
Wanafunzi wakatunga wimbo mzuri kuiisifu wakaimba kwa matari na maringo waliimba.

Shule yetu nzuri Mtakujaaa🎶
Mazingira twayatunza🎼 ,
Shule yetu nzuri Mtakujaaa🎹
Mazingira twayapenda,
Tutapanda miti,
Tusiruke viunga,
Na mwalimu wetu Kachiruuu,🎶
Mchapakazi hodariii,
Katuonyesha njia,
Tuifuate kwa makinii.

Shule yetu nzuri Mtakuja,
Mazingira twayatunza ,
Shule yetu nzuri Mtakuja,
Mazingira twayapenda,
Nanyi nyote kwa pamoja,
Tujumuike kwa umoja,
Tutapanda miti na tusiruke viunga,
Na shule yetu yapendeza,🎺
Mazingira yavutia.🎶


Wimbo huu uliwapa motisha wanafunzi wa kufanya shughuli hii Kwa umaridadi mkubwa na waliipanda na kuizingatia kwa makini huku wakihakikisha kuwa inapata maji ya kutosha na kuipalilia dhidi ya magugu, baada ya miaka mitatu Mazingira ya Shule ya Mtakuja yalibadilika isivyo kifani.

Pia kwa walimu wale ambao hawakua na nidhamu Mwalimu Mkuu Kachiru aliwazingatia na kuhakikisha wamebadilika na kuachana na miondoko yao ambayo ilikuwa sio mizuri.

HITIMISHO
Na huyu ndiye Mwalimu Kachiru, Shujaa na Maliki wa Mtakuja Shule ya Msingi, aliipaiiza Mtakuja ikasikaka masikioni mwa watu nao watu sasa wanapenda kuja Mtakuja.
 
Upvote 11
Mtakuja ..ndio ipo wapi hyo shule mkúu
 
Back
Top Bottom