Ni project!! Watamiminika wengi tu.....Aliyekuwa Kada wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Peter Buhime amejiunga rasmi na Chama cha Ukombozi wa Umma (Chaumma), na kukabidhiwa kadi na Mkurugenzi wa Mawasiliano kwa Umma wa Chaumma, John Mrema katika Mji wa Biharamulo
Peter, aliyewahi kuwa mtia nia wa Ubunge Jimbo la Biharamilo kupitia CCM mwaka 2020. Kada huyo pia amewahi kuwa Katibu wa UVCCM, Kata ya Saranga, Kibamba jijini Dar es Salaam
Chanzo: Mwananchi_official
Nimeona taarifa kuwa Kuna wanaCCM watahamia Chaumma na kuwa wabunge na baadae kutengeneza Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni fake Ili kuwalaghai wazungu walete pesa. Kuchangia bajeti yetu tegemezi chini ya kiongozi wa Upinzani Bungeni Mbowe. Atakayekuwa mbunge wa kuteuliwa na Rais baadae ya kugombea Urais Chaumma.