Mindyou
JF-Expert Member
- Sep 2, 2024
- 1,869
- 4,877
Wakuu,
Hivi karibuni nimeona video moja ya Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Makambako, Hanana Mfikwa akizungumzia kutumia viongozi wa dini kuwahamasisha wananchi kwenda kupiga kura.
Mfikwa alisema kuwa viongozi wa dini watumie ushawishi "kuwaelimisha" wananchi kuhusu kushiriki kwenye Uchaguzi na moja ya kauli aliyotoa ni kuwa
"Kama mtu atakuwa hajaenda kuchagua au kuchaguliwa basi nafikiri hata kwa Mwenyezi Mungu atakuwa hajatenda haki"
Najua humu jukwaani kuna watu wana uelewa zaidi kuhusu mambo ya imani, hivi ni wapi imeandikwa kuwa mtu asiposhiriki kwenye uchaguzi ni kosa? Huo mstari unapatikana wapi?
Na kwanini viongozi wengi wa CCM wanapenda sana kuhusisha dini na siasa?