Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Wakuu
Tunajua msimamo wa Chama upo wazi, bila mabadiliko hakutakuwa na uchaguzi na hawatashiriki uchaguzi, huyu Mapunda imekuaje ametangaza nia wakati wenzake wanapaza sauti ya No Reform, No Election?
==
Kada wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Romanus Mapunda, ametangaza azma yake ya kugombea urais kupitia chama hicho katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 2025.
Mapunda, ambaye ni mkazi wa Kawe, Dar es Salaam, alitoa tamko hilo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari katika hoteli ya Heritage Cottage, iliyopo katika Manispaa ya Songea.
Soma: Mapunda achukua fomu, ajitosa kinyang’anyiro cha Uenyekiti CHADEMA, kumvaa Lissu
Akiwa na ari kubwa, Mapunda alisema hana sababu yoyote ya kutogombea nafasi hiyo na kwamba amejipanga kikamilifu kushiriki mchakato wa kuwania urais kupitia CHADEMA, akisubiri taratibu rasmi za chama.
"Nimeamua kutangaza wazi kuwa nitachukua fomu ya kugombea urais kupitia tiketi ya CHADEMA. Naomba ushirikiano kutoka kwa chama changu kwa sababu nina mpango wa kuleta mabadiliko makubwa ya maendeleo nchini. Nataka kuijenga Tanzania mpya yenye mwelekeo mzuri kwa wananchi," alisema Mapunda.
Chanzo: Nipashe
Pia, Soma
Tunajua msimamo wa Chama upo wazi, bila mabadiliko hakutakuwa na uchaguzi na hawatashiriki uchaguzi, huyu Mapunda imekuaje ametangaza nia wakati wenzake wanapaza sauti ya No Reform, No Election?
==
Kada wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Romanus Mapunda, ametangaza azma yake ya kugombea urais kupitia chama hicho katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 2025.
Soma: Mapunda achukua fomu, ajitosa kinyang’anyiro cha Uenyekiti CHADEMA, kumvaa Lissu
Akiwa na ari kubwa, Mapunda alisema hana sababu yoyote ya kutogombea nafasi hiyo na kwamba amejipanga kikamilifu kushiriki mchakato wa kuwania urais kupitia CHADEMA, akisubiri taratibu rasmi za chama.
"Nimeamua kutangaza wazi kuwa nitachukua fomu ya kugombea urais kupitia tiketi ya CHADEMA. Naomba ushirikiano kutoka kwa chama changu kwa sababu nina mpango wa kuleta mabadiliko makubwa ya maendeleo nchini. Nataka kuijenga Tanzania mpya yenye mwelekeo mzuri kwa wananchi," alisema Mapunda.
Chanzo: Nipashe
Pia, Soma
- Tundu Lissu: Hatutasusia Uchaguzi, tutazuia uchaguzi kwa nguvu ya Umma, sio bila mabadiliko hatutashiriki uchaguzi
- John Heche: Tukishindwa kuzuia Uchaguzi Mkuu, basi CHADEMA hatutashiriki
- John Heche: Tumeamua kuhakikisha kwamba uchaguzi haufanyiki. Tutawashirikisha Viongozi wa dini, mashirika ya kimataifa, balozi na NGO's