Mtoa Taarifa
JF-Expert Member
- Sep 21, 2024
- 213
- 671
Taarifa iliyotolewa na Mwanachana wa CHADEMA, Hilda Newton imeeleza kuwa kada wa chama hicho katika mji wa Tunduma, Steve Chalamila amevamiwa nyumbani kwake na kuuawa na wanaodaiwa kuwa Green Guard.
Amendika kupitia mtandao wa X "tumepata msiba mkubwa Kamanda wetu Stivu Chalamila ameuwawa usiku wa leo baada ya watu wanao sadikika kuwa ni green guard kumvamia nyumbani kwake wakavunja mlango na kumkata kata sehemu mbali mbali za mwili wake na kupelekea kupoteza maisha.”-; Frank Mwakajoka.
-----
Kada wa CHADEMA Stephano Evaristo Chalamila mwenye umri wa miaka 23, ambaye pia ni ofisa wa chama Kata na mkazi wa kijiji cha Chapwa A wilaya ya Momba mkoani Songwe, ameuawa usiku wa kuamkia leo Novemba 27, 2024, baada ya kuvamiwa na watu wasiojulikana nyumbani akiwa amelala na kukatwa na kitu chenye ncha kali kichwani na mkononi.
Mwenyekiti wa baraza la wazee jimbo la Tunduma Ally Mwafongo, amesema kuwa marehemu ambaye ni afisa wa chama kata alivamiwa nyumbani kwake majira ya usiku na kukatwa na vitu vyenye ncha kali.
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Songwe SACP Agustino Senga, amesema hadi sasa wanamshikilia mtu mmoja ambaye ni bodaboda kwa ajili ya mahojiano ili kujua chanzo cha tukio hilo pamoja na wale waliohusika.