Kadampinzani asema: MBOWE AHOJIWE!

Status
Not open for further replies.

Mtetezi wa ufisadi huyo unadhani atakujibu hapa, umesoma chochote siku za karibuni akipondea wizi wa ccm na ufisadi wao? Huyu kuanzia atangaze rasmi kuwa upande wa mafisadi amekuwa hakemei chochote kuhusu ufisadi.

Mimi nawashauri ccm wamfungulie kesi Mbowe ili yote yaliyo sirini yaje wazi na ijulikane kama kweli huyo Ballali amekufa au la.
 

again, sidhani kadampinzani ni talk of the thread. Hapa anayeongelewa ni mbowe na kauli alizotoa. kwa kweli ni maneno mazito sana na tena nakushauri usome tena nilichosema !

Nilichosema ni kwamba, hao mafisadi ni kweli wapo, na sikatai ! Lakini iweje mashuhuda wakuu wa hizo kesi waendelee kuuliwa ili hali Mbowe amekiri hadharani kwamba wanauliwa na ccm halafu hapa tusitake mbowe ahojiwe kwa manufaa ya umma wa watanzania ili hao mashuhuda wasiuliwa na hao wanaccm ili wakamatwe na sheria ifuate mkondo ? Nilichokosea mimi ni nini ?? Kugundulika njia inayotumika kuwaua hao mashuhuda wakuu wa ufisadi au nini haswa nilichokosea, naomba uniambie !

Au wewe huoni kwamba, iwapo hawa mashuhuda (mfano: Ballali na amina chifupa ambao mbowe anadai wameuliwa na ccm) wangekuwa hai tusingepiga hatua kweli katika kuhakiki ufisadi unakomeshwa ? au wewe unafurahia kwa kuwa leo hii sauti za hawa mashuhuda zimesimamishwa na katu hazitosikika tena ?? ni kipi hasa unachojaribu kusema kwamba nimekosea !

Najua Mgaya tuna tofauti, hilo ni jambo la kueleweka. Lakini lets put that bullsh*t to the side, maana your argument is a silly argument in a serious situation !

Huoni kwamba mbowe ata-speed up na kuwapa moyo watu wenye ushahidi na kuwapa moyo wa kuwaanika mafisadi kwa wale wasiokuwa na moyo wa kufanya hivyo kwa kuogopa kuuliwa ??

Hivyo hadi hapo sina cha kuongeza, bali ninachopropose hapa ni Mbowe kuhojiwa !! hili sio suala la kisiasa, kichama, bali ni suala la usalama na manufaa kwa mashuhuda wa ufisadi !
 

Ha ha haaaaaaaa! Mi confidence ya nguvu! Nimekubali.

Labda kwa sababu itaibua 'masoo' mengine. Lakini kama kesi iki focus kwenye kifo cha Ballali, Mbowe ngoma yake inaweza kuwa ngumu!
 

tatizo lako ndio hilo, hili suala sio kuhusu ccm as the way you see it ! Lakini hadi utakapofika mbele na kuelewa ninachosema, ndio utajua nilichokuwa najua !

Na pia nadhani utakuwa hunitendei haki unaposema sitetei ufisadi ! Hayo ni maoni yako, and you have every right to express your thoughts, but they are dead-wrong thoughts ! i'll be happy if you trash those thoughts and carry on new ideas.

Bado tu hutaki mbowe ahojiwe ili watu wasitishiwe maisha yao katika kuhakikisha wapo salama ??
 
Ha ha haaaaaaaa! Mi confidence ya nguvu! Nimekubali.

Labda kwa sababu itaibua 'masoo' mengine. Lakini kama kesi iki focus kwenye kifo cha Ballali, Mbowe ngoma yake inaweza kuwa ngumu!

Nadhani Mgaya na wengi ndani humu hawajaelewa nilichomaanisha ! Hapa sio kufungua "case kuwa against na mbowe".. bali ni mahojiano ambayo yanatakiwa yafanyike ili ijulikane/kuiweka kikomo njia inayotumika kuuwa viongozi ambayo MBOWE amesema imetumika na ccm kuwauwa amina chifupa na ballali ! now people are getting things all twisted up, sijui kuwa against na mbowe! thats what they say, but what am saying ni kwamba mbowe ahojiwe kuhusiana na kauli zake kwamba amina chifupa, na akina ballali wameuliwa.. na akasema watauana zaidi hadi wamalizane ! wakimalizana will that solve anything for us tznians ? NO, sasa before hawajamalizana, nitafutahi kwanza watambulike na njia inayotumika kuua hao viongozi ili "chetu" kirudishwe then kama watataka kuuana they can go ahead !
 

hahaaa ! endelea kuchangamsha barza !
 
Lakini kama ukisoma mwanzo wa post ya Kada utagundua kwamba ana nia nzuri tu na Watanzania kwa ujumla.Yeye anachopendekeza ni kwamba Mbowe asihojiwe kwa ubaya ila atuambie sisi watanzania hao mafisadi(CCM par say) wanatumia mbinu gani kuua watu ili tuziweke wazi na hatimae kuzuia vifo vingine vya raia wema visitokee
 

Wewe ni fisadi tu na hilo nitalisema hapa mpaka jua likichwa na kuzama.

Kweli kabisa, Mbowe ahojiwe kabla wezi wa EPA na BOT hawajahojiwa? Mbowe ahojiwe kabla mhusika wa Richmond na Kiwira ajahojiwa, Mbowe ahojiwa kabla mhusika wa Buzwagi ajahojiwa? Mbowe ahojiwe kabla yule aliyenunua ndege mbovu ya raisi ajahojiwa?

Wewe kweli ni fisadi hadi kwenye damu, humuogopi mungu wewe?
 

ALikuwa na nia gani nzuri zaidi ya kupoteza mwelekeo, nchi inalia kwa IPTL, richmond, EPA, Kiwira , BUzwagi nk na wewe na wenzako huko ufisadi wa ccm mnaona kuwa MBowe ndiye prioriity?
 
Ha ha haaaaaaaa! Mi confidence ya nguvu! Nimekubali.

Labda kwa sababu itaibua 'masoo' mengine. Lakini kama kesi iki focus kwenye kifo cha Ballali, Mbowe ngoma yake inaweza kuwa ngumu!

Mimi nawashauri ccm wafuate ushauri wa fisadi mwenzao kada na kumhoji au kumfungulia mashitaka Mbowe kwenye hii issue ya Balali.
 
Kada,

Dakika chache zilizopita nimekupatia short list ya baadhi ya viongozi walioshikilia "sensitive issues" vichwani mwao ambazo zinasumbua vichwa vya Wadanganyika wengi, mimi nikiwemo. Ingawa hiyo listi haijaandikwa chronologically, but I think kuna mambo mengi ambayo yametokea tangu uongozi wa sasa uingie madarakani.

Mimi swali langu ni moja tu; Dont you think that viongozi wa Wadanganyika wangehojiwa (kwa kufuatia mfumo wa "first come - first served") kulingana na matukio yalivyotokea? By the time tunamfikia Mbowe ambaye katupa taarifa hizi masaa machache yaliyopita tutakuwa tumewatendea mema wadanganyika. Wewe unaonaje kwa hili?
 

Fisadi wewe nani atakuelewa?

Ukidai kuwa wezi wa richmonduli, buzwagi, epa, kiwira, rada, ndege na mengine yote wahojiwe utaeleweka zaidi.

Waambie wafungue kesi kama wataweza, laana ya mungu itakuwa juu ya mafisadi na watetezi hao.
 
Kazi kweli kweli naona mambo ya touchy, mushy,
 

je wakihojiwa hao viongozi uliowataja then MASHAHIDI wakahitajika ili kesi iendelee, keep in mind mbowe kasema hao watu waliouliwa ni kwa sababu walikuwa na ushahidi ! JE HAO MASHAHIDI WAKIULIWA HUKU CASE IKO PENDING STILL, huoni huo ndo utakuwa mwisho wa EPA,KIWIRA, RICHMOND na shabagalagala zoooote hizo ?? Hapo tutailaumu tena ccm kwamba imeua mashahidi ili hali tunajua kwamba mbowe anajua zaidi kwamba ni ccm inaoua hao mashahidi ??

Umesema mengi muhimu, lakini its just a matter of configuration, which goes first and what comes next ! Akihojiwa mbowe then hayo uliyosema yatafuata smoothly !
 

Wewew mtoto acha utoto ama waone washauri na madaktari wako wa akili wakupime.Hivi wewe una mtindio wa akili nini??Yani wewe hupati cha kuandika hadi Mbowe aseme??Acha utoto bwana unabore na ushamba wako.Yani unafikiri watu wanakufurahia??tumekuchoka bwana mdogo.
 

Sidhani kama ana jibu la hakika kwenye hili,

Yuko obsessed na Mbowe, soma signature yake.
Yuko kwenye kazi ya kumshambulia Mbowe na CHadema hapa kwa kila wanachofanya. Yeye hana uchungu kabisa na maisha ya watanzania.
 

Mafisadi wamehojiwa wangapi mpaka sasa? , kuna kazi nyingi za kufanya kabla ya kufikiria hili la mbowe Mkuu. Hivi kwa nini hawakumhoji Balali akiwa tanzania wakati ule badala yake wakaunda tume wakati majibu walikuwa nayo?

Kuna kipya alichokitoa ern&yng au ni yale yale yaliyokuwa tayari yanaeleweka? waambie wasipoteze muda wa kujiongezea kazi wakati zile za zamani zimewashindA.
 

Ok ! not a bad idea ! lakini wakihojiwa hao kwanza, then watu wanaotakiwa kujustify kama hizo claims ni za kweli au la, then mmoja baaada ya mwingine katika hao mashahidi wakaanza kudedi na case zikaturn COLD, ITAKUWAJE HAPO ?? maana hili la ballali mzee, trust me, the sh*t will go cold like it never happened !
 

Mafisadi hata mjaribu kubadili kasi ya watanzania kudai haki zao hamtafanikiwa. Wana JF hapa watakushambulia hadi ushangae.

Watu wamechoka na ufisadi wa ccm na wewe na wenzako lazima mjue hilo sasa. Wakati wa zidumu fikra za mwenyekiti wa ccm umepita.
 
ALikuwa na nia gani nzuri zaidi ya kupoteza mwelekeo, nchi inalia kwa IPTL, richmond, EPA, Kiwira , BUzwagi nk na wewe na wenzako huko ufisadi wa ccm mnaona kuwa MBowe ndiye prioriity?


Kumbe nimeshajua wapi umepotoka sio kila mtu anaekuwa tofauti na wewe ni CCM, nmechangia thread hii kwa sababu nimeona kada ana point

We fikiria kama kila anejua siri ya ufisadi akiwa anauwawa hizo priorities za buzwagi, IPTL, richmond and so on ni nani atazisimamia?

Muache Mbowe aseme hizo njia za mauaji zinazo tumika ili tuzizuie na tuendelee kuwaweka wazi mafisadi bila ya kuogopa kuuwawa!
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…