Kadampinzani asema: MBOWE AHOJIWE!

Status
Not open for further replies.
right on point ! lakini keep in mind sio mafisadi tu, bali hata hao wanaouwa mashahidi dhidi ya ufisadi !

CCM mnaua watoto wachanga, wakina mama wajawazito, wanafunzi masikini, wazee wastaafu kwa wizi na ufisadi uliokithiri na bado hayo yote hujayaona na umemwona MBowe tu!

Unapambana na mungu katika hili na nakuhakikishia kuwa mbinu zako zote zitashindwa kama ambavyo umeshindwa kila mara hapa JF kutetea ufisadi.
 
Wewe kada hayo ya mbowe ni ya lini mbona hujawahi kuanzisha thread ya watu wa EPA, KIWIRA nk wahojiwe?

kwa hiyo kupinga ni lazima uanzishe thread au una maanga gani ??? mbona unanichekesha mzee !

3 ways to change things !

(a) you can change it yourself.
(b) if you cant change it yourself, speak about it - WHICH I DID
(c) if you cant speak about it - then FEEL BAD ABOUT IT !

wewe ulitaka nifanye kipi kingine hapo juu ??
 
Wewe kada hayo ya mbowe ni ya lini mbona hujawahi kuanzisha thread ya watu wa EPA, KIWIRA nk wahojiwe?

Unadhani ataweza hili?

Subiri uone atakuja na udaku mwingine wa kuhusu Mbowe na Dr Slaa kama kawaida yake.
 

Unaambiwa mbowe ameongoe ki JF JF huna haja ya kwenda mbali. Polisi hawana muda na mbowe kuna shughuli nyingi zinazomaliza taifa ambazo wanatakiwa washugulikie.
 

Kakindomaster,
Watanzania sio wajinga hata siku moja, wakati Kikwete mambo yanamwia magumu wananchi wanaangalia the next move. Sasa kama Mbowe is next lazima awe anaongea mambo yanaoonyesha utashi wa uongozi ambao atakuanao pale atakapo chaguliwa.

Sasa kama leo hii Mbowe anasema kila kiongozi aliekufa kauliwa na viongozi hata pale madaktari wanapothibitisha vinginevyo na kama Mbowe kwa tamaa zake za uongozi yupo tayari kuubadirisha ukweli uliothibitika ni juu ya wananchi kuhoji suitability yake kama rais.

Sina visa na Mbowe, ila maoni yangu binafsi ni kwamba Zitto na yule dogo Mnyika wana nafasi kubwa ya kukifanya Chadema kuwa chama madhubuti...ungozi ni pamoja na kuchagua maneno na vyazo vya habari...jambo ambalo linamshinda Mbowe.....just my opinion
 

Kwani wakati unaanzisha hii ulikuwa namaana gani?
 
usije ukakimbia tu !

Hapa kuna wanachama wengi sana hawaipendi ccm na ufisadi wake na mimi ni only part ya process. Wewe na wenzako ndio mtakimbia hapa au mtakiona kijiwe cha moto kama ilivyo sasa hivi ambapo ufisadi wenu unaanikwa kama kawaida.
 

Nimekuelewa vizuri, ila nadhani ni kumuonea Mbowe kutaka ashurutishwe kuhojiwa na dola. Tukisema kwamba watu wote wanaosema vitu vyenye utata hadharani wahojiwe na dola, nchi inaweza kugeuka Police State ya kamata kamata. We do not wanna go there (or go back there - wakati wa Nyerere hako ka tabia kalikuwepo).

Ndio maana nikapendekeza CCM wamshitaki. Hii wewe unadhani sio mada hapa, lakini kama nia yako ni kupata ukweli wa nini anacho kijua Mbowe nilitegemea ungeiona hii pia ni viable alternative. Hii ya kumfuata na dola inaelekea kwenye mambo ya Criminal case ambayo kwa kweli ni kama kumnyima haki zake za kuongea huru. CCM wakimshtaki inakuwa kesi binafsi, na siyo ya dola. Kwa hiyo unakuwa ume balance pursuit of truth against Civil liberties za Mbowe. Na kama akikutwa hana vidhibiti siku nyingine atakoma kupiga mayowe ya uwongo.

Kwa hiyo, nilikuelewa vizuri, ila nikapendekeza njia nyingine itakayo tupeleka kule kule kwenye lengo lako zuri sana la kuwatambua wahusika "kabla hawajamalizana."
 

NAKUUNGA MKONO 100% KWA 100% NA HIYO NDIYO KAULI ALIYOTOA MBOWE ! BUT HE HAD MORE DETAILS THAN YOU !

NOW WHAT AM SUGGESTING IS, MBOWE DID THE RIGHT THING BY POINTING THAT OUT, LAKINI SASA KAMA CCM WANAUA HAO ULIOWASEMA, IS HE DONE BY SAYING WHAT HE SAID ?? SHOULDNT HE BE ASKED AND START PIN POINTING EVERYTHING OUT RATHER THAN SAYING ALONE ??

NAONA UNAANZA KUELEWA TARATIBU, BUT I'LL BE PATIENT WILL YOU UNTILL YOU GET IT ! MAANA MTOTO MCHANGA HAZALIWI AKITEMBEA !

YOU'LL SOON GET WHAT AM TALKING ABOUT !
 

Alichosema Mbowe ni maoni ambayo hata hapa JF wengi wameyasema. Issue ya Balali imejaa usanii wa hali ya juu na hili lazima lisemwe.

Kama mafisadi huko ccm mlidhani kuwa mmepata cha kutokea hapa basi tayari mmechemka kuanzia mwanzo. Mtabana kama Mkapa na baadaye mtaanza kusema kadri siku zinavyoendelea.
 

Mbowe anaongea mambo mengi na hawezi kuongea namna wewe na mafisadi mnavyomtaka aseme. Hii issue ya kifo cha Balali na kile cha Chifupa kimezua maswali mengi na lazima MBowe atoe mawazo yake kwenye hili.

Zaidi ya hapa bado nakushaurini mmshitaki Mbowe ili muone kitakachotokea.

BTW, kuandika kwa CAP kunamaanisha kupayuka (kwenye mitandao).
 

Nami nimekuelewa vizuri, lakini lazima tuangalie hili suala kiundani ! Hao wanaoliwa hawauliwi kwa sababu ya ccm, bali kwa sababu ya taifa ! wanahujumu mali za taifa na sio ccm !

sasa suala la kusema kwamba ccm ifungue kesi kwa kitu ambacho ni kwa ajili ya manufaa ya taifa, that statement doesnt seem to be right to me. Hivi kwa mfano usalama wa taifa ukiwa mashakani, unataka kuniambia ccm ndio wanaotakiwa kufungua kesi/kushughulikia hilo suala na sio taifa ??

keep in mind, hili suala sio kuhusu upinzani wala ccm ! bali watanzania wote !

Mbowe ahojiwe !
 

Sasa Mkuu si hao wenye ushahidi wawaambie watanzania?. Wakati mwingine maneno mengine yanasemwa baada ya wahusika kukaa kimya. Si unaona leo na mkapa agalau kanena? mangapi yameisha semwa?

Yote yanatokea kwa sababu viongozi hawataki kutoa majibu sahii pale wanapotakiwa kufanya hivyo. waliniambiwa JKT kuwa ukimuona mtu amekaa kimya hili kupata ukweli mchokonoe. Sasa mbowe alichofanya ni kuchokonoa hili mwenye ukweli basi atwambie tu.
 

nakumbuka nilipokuwa darasa la kwanza, siku ya kwanza darasani, kuna dogo nilimsikia akimwambia mwenzake maneno kama hayo uliyosema ! kama utaelewa ninachomaanisha haya ~!
 
Alichosema Mbowe ni maoni ambayo hata hapa JF wengi wameyasema. Issue ya Balali imejaa usanii wa hali ya juu na hili lazima lisemwe.

Kosa # 1. Sio kila linalosemwa na wengi lina ushahidi na hivyo ungetegemea kiongozi wa kitaifa kama Mbowe kulijuwa hili na kuwa makini.

Sioni haja ya Mbowe kuhojiwa kwa hili, ila kauli zake mara nyingi zinanifanya ni -question uwezo wake wa kuongoza Tz kama rais.
 
nakumbuka nilipokuwa darasa la kwanza, siku ya kwanza darasani, kuna dogo nilimsikia akimwambia mwenzake maneno kama hayo uliyosema ! kama utaelewa ninachomaanisha haya ~!

Yashakushinda na umeanza kuja na mifano ya darasa la kwanza. Ama kweli kutetea ufisadi ni laana hadi uwezo wa kufikiri unakwisha kabisaaa.

Hivi ccm hawana mtu mwingine bora wa kuwatetea hapa?
 

ukweli mtupu !
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…