realMamy
JF-Expert Member
- Apr 28, 2024
- 3,925
- 8,853
Hii iko wazi kuwa Mtoto wa Kike anakumbana na Vikwazo vingi sana hadi kutimiza ndoto zake. Vikwazo hivo huanzia Pale tu anapozaliwa katika familia ambazo zilihitaji Mtoto wa Kiume kuwa wa Kwanza ili kupata mtoto wa kuendeleza ukoo na kurithi mali.
Basi huanza kubaguliwa kuanzia hapo yeye na mama yake na hata mitandaoni tunasoma story nyingi tu zinazohusu ubaguzi wa mtoto wa kike.
Ngazi nyingine anayokumbana na Kikwazo ni Shuleni pale anapowekwa kuwa Msaidizi wa kila kitu na Si kiongozi. Shuleni pia atakumbana na Changamoto za kimahusiano na watu wazima na hata kutishiwa pia kuwa asipofanya hiki anaweza asipate kile Mfano Chuoni.
Na hata Ngazi za Chini pia tumesikia kwenye taarifa za habari kuhusu watoto wa kike wanaopitia ukatili. Tuje kwenye suala la kutimiza ndoto zao baada ya Kuhitimu Masomo.
Ofisini pia kuna ukatili unaofanywa na Baadhi ya Mabosi wengi wa Kiume humpa mtoto wa kike masharti ili aweze kupata kazi.
Hii huumiza sana kiukweli na kumfanya mtu ashindwe kufanya kazi kwa amani na ufanisi.
Vivyo hivyo kwenye Vipaji ili uweze kutoka lazima ukutane na ukatili wa Kingono la sivyo hufanikiwi. Kwenye suala la Siasa pia Mtoto wa kike anakumbana na Changamoto ya kuaminika kuwa anaweza kuwa kiongozi ingawa kwa sasa hali inaendelea kuimarika.
Kuna mambo mengi tu yanayofanya mtoto wa kike kushindwa kutimiza malengo yake na hata ikitokea ametimiza basi wengi watajiuliza amewezaje.
Tumpe nafasi na tumuamini Mtoto wa Kike anaweza.