KERO Kadhia wanazopata Wafanyabiashara Mbezi Stand ya daladala ya juu

KERO Kadhia wanazopata Wafanyabiashara Mbezi Stand ya daladala ya juu

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Leo hii nimeamua, kushika kalamu kuandika hili kwamba wafanyabiashara wadogowadogo waliopo Mbezi wanapata kadhia sana kwenye kufanya shughuli zao za kila siku, ila wenye taabu kubwa ni wafanyabiashara wa ice cream (ukwaju) wanapata kadhia wakiwa katika stendi ya daladala ya juu kutoka kwa Wanausalama wa Suma JkT.

Kwa ukweli ukiangalia kweli kuna tangazo eneo lile haliruhusiwi mtu kufanya biashara ni kweli, kitu kinachouma hata Wafanyabiashara wa ice cream wakiwa pembani ya eneo hilo SUA hawakimbiza na kuwakamatia mizigo ambacho sio kitu sahihi na kama ni sahihi waoo wamekosea kwani udai hongo ili wachie mizigo yao.

Tena huwapa vitisho vikali na kuanza kula ice cream zao kwa dharau je hii ni haki kutumia cheo ulichonacho kama fimbo?

Na kwa tabia zao za kupendwa kuongwa ili wachie mizigo washawaona wauza ukwaju kwao kama fursa.

Jamani tunaomba hili lishughulikiwe na wafanyabiashara wadogo wadogo wapewe maeneo muhimu ya kufanyia biashara zao kama tuanavyoimizwa kujiajiri na sisi tupewe mazingira rafiki ya kufanyia biashara.

Asante
 
Back
Top Bottom