Kadi ya NIDA inakitu gani special hadi iwe ngumu kuprint kiasi hiki? Passport na NIDA kipi kigumu kuchapisha?

Kadi ya NIDA inakitu gani special hadi iwe ngumu kuprint kiasi hiki? Passport na NIDA kipi kigumu kuchapisha?

Resilience

JF-Expert Member
Joined
Jan 4, 2023
Posts
1,096
Reaction score
4,948
Passport ya Tanzania unapata ndani ya siku moja baada data kuingizwa kwenye mtambo. Benki kadi unapata ndani ya masaa kadhaa, najiuliza hii kadi ya NIDA ina teknolojia gani ngumu hadi ukae mwaka bila kuprint kitambulisho?

Lakini kama wenye namba ya NIDA wanapata huduma zote kwanini tunaamini tunahitaji uwekezaji mkubwa kwenye Vitambulisho? Kwanini wananchi wasiachwe wakaprint kwenye pvc cards kama zamani kupunguza gharama za serikali?

Ukiwa na namba means una ID, tubadili fikra teknolojia inabadilika sana. Tuondoe viongozi mzigo ,naamini Mchechu akienda NIDA au wakipata waziri kama Bashe hili tatizo litaisha
 
Wewe wazungumzia mwaka tu
Kuna watu tuna miaka tangu kipindi zoezi linaanza mpaka leo tunatumia namba tu kila ukienda kwenye kata husika wanachambua unaambiwa havijafika
Cha ajabu kuna waliojiandikisha mwaka huu na wameshapata
 
ufala tu mwingi

kwanza hata update ya Data zetu ni shida! mtu alijaza miaka 13 imepita
 
mwaka wa 6 huu unakatika, ukiwapigia wanakwambia bado
 
Mimi nilijiandikisha kupata nida mwaka 2012 wakati huo nipo jkt, mpaka leo 2023 sijapata kitambulisho zaidi ya namba. Ajabu passport nimeipata ndani ya siku 4 tu tena bila longolongo wala hongo.
 
Passport ya Tanzania unapata ndani ya siku moja baada data kuingizwa kwenye mtambo. Benki kadi unapata ndani ya masaa kadhaa, najiuliza hii kadi ya NIDA ina teknolojia gani ngumu hadi ukae mwaka bila kuprint kitambulisho?

Lakini kama wenye namba ya NIDA wanapata huduma zote kwanini tunaamini tunahitaji uwekezaji mkubwa kwenye Vitambulisho? Kwanini wananchi wasiachwe wakaprint kwenye pvc cards kama zamani kupunguza gharama za serikali?

Ukiwa na namba means una ID, tubadili fikra teknolojia inabadilika sana. Tuondoe viongozi mzigo ,naamini Mchechu akienda NIDA au wakipata waziri kama Bashe hili tatizo litaisha
Haina ugumu wowote

Tena infact infrasture ya kujenga Passport ni more complicated na expensive zaidi ya NIDA

Sasa sababu ni hii:

1)NIDA vinatolewa BURE,serikali haina HELA ya kugharamia watu milioni 60 NIDA za bure zote
2)Passport kila mtu analipia ghali na sababu ya kipato,vifaa na kila kitu vinapatikana kwa faida na fasta

Hapa ni monetary incentive ya kujenga hivi vitambulisho viwili tu ndio sababu

Serikali haina hela wala UWEZO wa kutoa NIDA BURE nchi nzima,hivyo mashine ni chache na duni,manpower ni ndogo,bajeti ni 0 hivyo NIDA mpaka tunakufa itakua ni shida tupu unless walete mpango wa kulipia kama Passport.

Na wakileta mpango wa kulipia kama Passport hakuna mtu ataenda kulipia maana 80% ya nchi ni masikini,hawawezi!

Ndio maana Passport wanapata watu wenye uwezo wa kulipia wenye kipato cha juu kwenye jamii....Tanzania sidhani wenye passport za kusafiria nje wanazidi 10% ya population.
 
Back
Top Bottom