bobishimkali
Member
- Aug 25, 2010
- 59
- 0
Hivi inawezekanaje kadi zote ziwe mpya kiasi hiki? Kadi nyingi ukiziona kawaida baada ya muda huwa zina-fade au kuchakaa kidogo!! Sasa hizi je, imekuwaje? Kanyaboya lingine hilo.
JK kadanganywa tena kadi zote mpya yeye hata hajiulizi inakuwaje kadi zote ziwe hazijakunjwa na namba zinafuatana
A serious note! Raisi wetu ni mgonjwa wale wa kwenye fani ya afya wanaweza kubaliana nami, hana mng'alo wa mtu aliye mzima inawezekana amechoka ama ametindikiwa na msongo wa mawazo. Take a rest Mr Predidaaa
Hali ilivyo hadi sasa CHADEMA wanayo nafasi kubwa ya kuyachukua majimbo ya Mbeya Mjini na Mbozi Magharibi, wanachotakiwa kufanya ni kuelekeza nguvu zao huko kwa kuwasaidia wagombea wao, wasiwaache wajitegemee kwani CCM wanalielewa hilo hivyo watajiandaa kwa ghiliba zozote zile
A serious note! Raisi wetu ni mgonjwa wale wa kwenye fani ya afya wanaweza kubaliana nami, hana mng'alo wa mtu aliye mzima inawezekana amechoka ama ametindikiwa na msongo wa mawazo. Take a rest Mr Predidaaa
MKUU REV MAS
Kwani mabango ya JK ambayo yamesambazwa dar es salaam ukiangalia vizuri PICHA ZAKE ZINAONESHA MUNGARO WA AINA YAKE?
jE MPIGA PICHA ALIKOSEA?
Kiongozi picha za kwenye Mabango zimefanyiwa nakshi na brushing! hizi za sasa zinatoka kama alivyo kwenye uhalisia
SASA na hii si imefanyiwa brushing? au ndo muonekano wake kwa sasa?
mwaka jana wampige mawe kiwete.....leo hii warudisha kadi..?
Kwa kipi alichowafanyia..? Ingekuwa bagamoyo sawa..! Sio mbeya..!
Asante sana Nsesi! Usiwe unapotea sana hasa kipindi hiki
Tatizo la JK ni sifa na wasaidizi wake wanalielewa hilo. Ule mchezo wa Mbalizi kafanyiwa na viongozi wa CCM Mbeya katika kujipendekeza kwa kwa bosi wao. Wanafahamu fika kwamba Mbalizi ni ngome ya CHADEMA hivi sasa kama ilivyo Tunduma, kwa hiyo kuonekana wamefanyakazi walitengeza usanii wa kubomoa ngome ya chadema pale Mbalizi.
Seme na wenzake walishindwa kwenye chaguzi halali, hivyo sio vingozi tena na kujiondoa kwake chadema kulisharipotiwa siku nyingi kwa hiyo haikuwa habari tena, na hata alipotambulishwa kwenye mkutano ule wananchi waliguna.
Katika kumuonyesha JK kwamba wao hawababaishwi, wananchi walikaa kimya hata alipotambulishwa mgombea ubunge Mch. Mwanjale.