Kadiri siku zinavyokwenda unawaona gen z Kenya wanafanikiwa mahitaji yao au wanapoteza malengo na uelekeo wa madai yao kwa serikali ya Kenya?

Tlaatlaah

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2023
Posts
24,665
Reaction score
25,388
Kudinda kwao kua na mazungumzo na viongozi wa serikali ikiwa ni pamoja na Rais mwenyewe William Samoe Ruto alietoa wito wa majadiliano tangu mapema sana mwa mwanzo wa maandamano yao..

Lakini pia dhana ya kwamba wao hawana viongozi, huku pia wakiwakataa wanaojiita viongozi wao wanayojaribu kukutana na waandamizi serikalini, hii si dalili ya migawanyiko miongoni mwao na hatimae mwanzo wa kupoteza lengo la mapambano ya mahitaji yao..

Kuna wale wanaoimba Ruto must go now. na kuna wale wanao apa kwamba Ruto ni one term president, mwisho wake ni 2027, hii pia si dalili dhahiri ya kuanza kugawanyika na hatimae kupoteza lengo na uelekeo wao?

Kuna upande wa nchi ya Kenya, hivi sasa wanajipiga kifua na wanadai watamlinda mtoto wao kwenye uongozi wake, hawata kubali abanduliwe mamlakani. Je, huu si ukabila unabisha hodi kwenye harakati hizi za vijana na kubadili kabisa sura na makusudi ya mapambano ya vijana?

Serikali ya Kenya inafanya mabadiliko makubwa sana ya kiutawala, kiutendaji, kubana na matumizi kulingana na inavyoona inafaa, japo kwa kiasi fulani mageuzi hayo yanaakisi madai ya gen z , ingawa wenyewe hawamo kwenye meza ya mazungumzo kushuhudia na kusimamia mabadiliko hayo yapate nguvu zaidi na ili yalete matokeo chanya kwenye madai yao.

Kwa mwenendo wanao kwenda nao sasa na dalili za migawanyiko, kitisho na hatari za kusambaratika kwao kwa misingi ya kikabila na kikanda zinazo anza kudhihirika bayana miongoni mwao,

Unadhani wanaweza kufanikiwa azma yao kuidhibiti serikali na malengo yao kutimiziwa ili hali hawataki kuja mezani pamoja na serikali kwa mazungumzo?
 
Mimi naona wamefanikiwa Pakubwa, kwa sababu lengo Lao la mwanzo ambalo ndilo chanzo cha maandamano limetimia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…