JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Kufuatia uwepo wa malalamiko kutoka kwa baadhi ya wananchi ambao hasa wanapakana na maeneo ambapo inapita Reli ya SGR kudai uwepo wa umbali katika Vivuko vya kuvukia baina ya kimoja na kingine, Mkurugenzi wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Masanja Kadogosa amekili uwepo wa changamoto hiyo na kudai kuwa tayari jitihada za kuleta ufumbuzi zimeanza kufanyika.
Hoja ya malalamiko ya kukosekana kwa kivuko, ipo hapa ~ Wananchi tunateseka kupita kwenye Kalavati kuvuka eneo la Reli ya SGR Mitaa ya Banana
Masanja Kadogosa anasema "Ni tatizo hatuhitaji kuanza kusingiziana sijui nini mchawi ni nani, ni kutafuta suluhisho."
Amefafanua kwamba awali kabla ya ujenzi wa reli hiyo walishirikisha Wananchi pamoja na viongozi wao na wakakubali vivuko viwekwe maeneo yapi, lakini amedai huenda walijua ujenzi utakuwa kama wa Reli kawaida ambapo wamezoea kukatiza.
"Tulipo dizaini Mwaka 2017 Wananchi wote walishirikishwa na sio tu kwa kushirikishwa na kwa kusaini, kwamba tumeridhia kivuko cha kwanza kikae hapa na kingine hapa. Wenyewe walifikiria itakuwa kama Reli ya zamani kwamba wangeruhusiwa kupita juu," amesema.
Ameongeza "Walikuwa wanasema weka hapo na hapo bila kujua vile Vivuko watatumia wao, tumekuja kuweka fansi imeleta matatizo."
Kufuatia kubaini changamoto hiyo amesema kuwa tayari licha ya uwepo wa vivuko ambavyo vipo kwa sasa, lakini ameweka wazi kuwa tayari wameshapitisha mchoro kwa ajili ya ujenzi wa Vivuko vingine ambavyo amesema vitaanza kujengwa hivi karibuni.
Amesema "Kwahiyo tumeshaweka vivuko kama vitano kama sikosei, viwili nafikiri vitakuwa Dar es Salaam kuna kimoja kitakuwa Kilosa na Kingine kipo Dodoma na Kingine kipo kipo Bai. Ujenzi wa Vivuko ni 'addition' inachukua muda, tumeshapitisha mchoro, nafikiri hivi karibuni wataanza ujenzi."
Itakumbukwa baadhi ya Wananchi wamekuwa wakidai kuwa umbali huo umekuwa kero kubwa kukatiza upande kutoka upande mmoja kwenda mwingine hasa kutokana na uwepo wa uzio, huku baadhi yao eneo la Banana wanalazimika kuvuka kupitia kalavati la maji ambalo sio rafiki kutumika kama njia.