Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Reli nchini (TRC), Masanja Kadogosa amesema viwanda zaidi ya 250 vinatarajiwa kujengwa eneo la Kwala, wilayani Kibaha Mkoani Pwani, ambapo amedai hatua hiyo inachangizwa na uwepo wa Treini ya kisasa ya (SGR) inayopita karibu na eneo hilo.
Kadogosa amesema kuwa wadau hao hata wakiwa wanajitangaza wanazingatia zaidi ukaribu uliopo kati ya eneo linalokusudiwa kujengwa viwanda na inapopita Treini ya SGR.
"Tunapozungumza sasa hivi pale Kwala kuna viwanda kama 250 vinakuja, na uki-google ukaangalia sehemu kubwa ya kujitangaza kwao wanazungumzia tuko ndani ya mita 500 ya SGR."amesema Kadogosa
Pia mesema kuwa licha ya viwanda hivyo pia tayari amepokea taarifa kwa hivi karibuni kuwa viwanda vingine 100 vinatarajiwa kujengwa maeneo mengine ambao yapo katika mwambo wa SGR inapopita.
Ameeleza kuwa mradi huo unavutia uwekezaji kwa kuwa utakuwa unatoa fursa ya wafanyabiashara kusafirisha kwa uharaka na urahisi mizigo yao kwenda maeneo mbalimbali nchini hadi nje ya Nchi kulingana na mradi huo unavyoendelea kutanuliwa, hivyo amewahasa vijana kutumia fursa za kiuchumi zilizopo, ambapo amedai kuwa vijana wakizembea itashuhudiwa mabilionea watakaonufaika na mradi huo wakitokea nje ya Nchi.
"Serikali kazi yake kubwa ni kutengeneza mazingira ya Watu kuweza kufikiri na kutengeneza pasa, ndiyo kazi ya Serikali. Na kwa uwekezaji mkubwa uliofanywa kwa utashi wa Rais wetu nafikiri hiyo kazi ameitimiza"amesema Kadogosa
Ameyasema hayo Julai 4, 2024 alipokuwa akizungumza na wanahabari kufuatia kutembelewa na baadhi ya viongozi wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi Taifa (UVCCM), wakiongozwa na Mwenyekiti wa UVCCM Taifa ambaye ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM ya Taifa, Mohammed Ali Kawaida na Katiba Mkuu umoja huo, Jokate Mwegelo pamoja wengine.
Ambapo kwa ummoja wao wametembelea kituo Kikuu kilichopo Dar es Salaam kana kuelezwa mambo mbalimbali ikiwemo utaratibu wa ukataji tiketi, pia wamefanya ziara kwa kutumia Treini kutokea Dar es Salaam kuelekea kituo cha Pungu
Akizungumzia ziara hiyo Mwenyekiti wa UVCCM amsema kuwa Rais Samia Suluhu Hassan alitoa maelekezo kuhusu kuanza safari za Treini, hivyo ziara yao TRC imelenga kukagua maelekezo ya Rais Samia ambaye ni Mwenyekiti wa CCM Taifa.
"Mh. Rais Samia Suluhu Hassan moja katika maelekezo yake kwa ndugu zetu TRC, aliwaelekeza inapofika Mwezi huu tayari TRC wawe wameanza safari zao za Treini, nasisi kwa kuwa ni viongozi wa Chama Cha Mapinduzi, kazi yetu kubwa ni kufuatilia utekelezaji wa Ilani na maelekezo ya Rais. Kwahiyo tulikuja kujilidhisha kwa kiasi gani TRC wametekeleza maadhimio au maelekezo ya Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi ambaye ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania"amesema Kawaida" amesema Kawaida
Aidha licha ya kuridhishwa na hatua hiyo ametoa wito kwa vijana kuwa msatari wa mbele kulinda miundombinu ya mradi huo na kuwa mstari wa mbele kuhakikisha unapiga hatua badala ya kukwamisha.
Licha ya kwamba tumefurahishwa mno na mradi huu, tunao wito wa kutoa kwa jamii na hususani kuhusu kundi kubwa la vijana, kundi hili limekuwa likitumika kwa namna moja hama nyingine kukwamisha, lakini kundi hili linapotumika vizuri ndilo kundi ambalo linaweza kufanya mambo haya yakenda kwa kasi zaidi.
Ikumbukwe Safari za awali za treni za SGR, kati ya Dar es Salaam na Morogoro zilianza rasmi Juni 14, 2024 ikiwa ni maandalizi ya kuanza rasmi kwa safari hizo Kati ya Dar es Salaam na Dodoma ifikapo Julai 25, 2024.