Kaduguga na Kassim Dewji lazima mkubali kuwa zama zenu zimeisha, kuondolewa kwenye bodi ya wakurugenzi Simba muda wowote

Mwishokambi

JF-Expert Member
Joined
Nov 23, 2020
Posts
390
Reaction score
1,425
Mwina Kaduguda maaarufu kama Simba wa Yuda ambaye amekuwa akijinasibu kuwa eti yeye ni Simba lia lia na yuko tayari kutolewa kafara endapo itatakiwa Simba awe bingwa wa afrika sasa amekalia kuti kavu kufuatia maneno yake ya hiv karibuni siku chache kabla ya mnyama hajacheza na Yanga nusu fainali ya ASFC kule Kirumba Mwanza.Kaduguda alionekana kwenye social media akidai kuwa anaiheshimu sana Yanga na hata kama ikitokea Wazee 10 tu wa yanga wakajiita wao ni yanga na wakataka kucheza soka basi shughuli ipo, Kaduguda aliipa nafasi yanga kuifunga Simba, hata alipoulizwa kama anakwenda kirumba alisema asingeweza kwenda kwa sababu yuko busy na biashara zake.

Baada ya Simba kubanduliwa na Yanga, akaibuka board member mkongwe kabisa ndani ya Simba, Kassim Dewji naye black and white, akaenda radio efm yenye popoma Maulid Kitenge akajiachia utadhani yuko na mkewe nyumbani, siri zote za bodi akaenda kumwambia kitenge pale efm, Kitenge anavyopendaga umbea basi akaona bonge la habari kwake.Leo tena imevuja clip Kassim Dewji akipewa makavu na mtu mmoja aliyejulikana kwa jina la Hussein kuwa anahujumu Simba.

Kwanza mimi nasema nakubali Kassim Dewji na Kaduguda ni wakongwe sana ndani ya Simba lakini walichokifanya kwa kweli ni usaliti mkubwa sana, Niliwahi kushauri hapa kuwa Mo Dewji aivunje bodi nzima, ondoa waswahili njaa wote hao akiwemo Asha Baraka, Simba haitakuwa na mafanikio yoyote kwa kuwa na watu hao, hao akina Kaduguga wanaodai wana mahaba sana na Simba hamna lolote, we uipende Simba halafu ikaribie kucheza na mtani unaanza kuvunja watu moyo halafu useme wewe una mapenzi na Simba.

Kaduguda, Asha Baraka, Kassim Dewji wakae pembeni, otherwise usaliti utaendea
 
Kaduguda alizengua kwakweli.
 
Kassim dewji aliweka million 300 vunja bei akafika billions 2 hadi leo hiko kitu kinamuuma sana bado ile millions 500 ya kupangisha jengo la simba kustukiwa
Juzi kwenye interview ile ya Efm alienda na jezi yenye nembo za UHL zile alizokuwa anasambaza yeye yaani hata kuvaa jezi mpya ya vunjabei hataki, hiyo tu inatosha kukuambia ana ajenda gani
kufungwa na utopolo na kukosa ubingwa watu wamefunguka aisee hawa watu wameumia sana kwa hii miaka 4 wamesubiri kaupenyo kadoogo kutaka kuleta vurugu sasa maskini ya Mungu mashabiki wamewapuuza
Kuhusu asha baraka nakuhakikishia huyo ana afadhali ya kipesa kuliko kaduguda,dewji sidhani hata kama ule mkahawa wa food world aliokuwa anautumia zamani kusainisha wachezaji kama bado upo, ka miss sana kuipiga simba kwenye jezi na rent ya jengo
kuhusu kaduguda huyo sijui kama ana kazi kwa kweli, naju alikuaga mwandishi alishawahi kuidai simba chapati alizokopesha wachezaji
bodi inabidi iwe na watu wasiokuwa na njaaa
 
Unamuonea bure Asha Baraka, hakuna baya amefanya.
Sijui kwanini unapania sana afukuzwe.

 
Kaduguda mwaka wa njaa huu alikuwa na meza ya kuuza dagaa pale sokoni kariakoo soko likaungua,sasa hana dili mjini
 
Hapo kwenye kuikopesha Simba chapati za wachezaji nimecheka Sana. Hivi hizo chapati alilipwa? Tuanzie hapo
 
Kassim Dewji nilikua namuheshimu na namkubali sana lakini tangia nilivyomsikia akiropoka hovyo EFM kazi na yeye imekwisha rasmi.
Simba kwanza mambo mengine baadae.
 
Kaduguda anajivunia uchawi tu ni mpuuzi sana
 
Kaduguda Yule n wa wanachama n ngumu kumfukuza hilo sahauni labda kasim
 
Ila yule kitenge ndo maana manara alimwambia sio riziki yeye huwa anawatafuta wazee wa simba tu ila wa yanga hawagusi .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…