nzalendo
JF-Expert Member
- May 26, 2009
- 12,106
- 12,916
Ni ndugu yangu.
Nilihangaika nae mpaka watu wakanishangaa,lakini haya niliyafanya ili wazee{wazazi}wasilemewe na mzigo.
Dogo huyu kwa sasa ni mtu mzima mwenye maisha yake ,alianza kidogo kidogo kunywa mbege wakati wa krismasi huko Moshi,akiwa darasa la tatu.
kabla ya kumaliza darasa la saba akawa tayari kushamudu bia n.k.
Form four bange, gongo n.k.
anamaliza chuo ni cha P
akapata kazi nzuri siku akilipwa anapotea wiki nzima ulevi ulevi ulevi.
kazini hadumu wanamtema,lakini cha ajabu huwa hakai kijiweni(bila kazi zaidi ya miezi 2-3)
Ana bahati sana ya kupata kazi lakini hadumu,kazunguka makampuni mengi nchi hii ya Tanzania.
Rafiki zake wamemzungusha kwa waganga wengi lakini haikusaidia kitu.
Akapata kazi shirika fulani la wazungu...wazungu wakampenda sana...wakaamua kumsaidia,manake kwa kazi jamaa ni jembe na ni kichwa hasa....lakini akigusa pombe tu;ni mtihani atataka kunywa na kunywa na kuvuta mpaka aishiwe tena anauza hata vitu vyake ili tu akalewe,Basi wazungu waka mpeleka 'sober house' mara kadhaa lakini haikusaidia.
Ameshazunguka kwenye makanisa ya mboga mboga na yasiyo ya mboga mboga.
watu wooote walimtenga ndugu jamaa na marafiki.
ALIPONAJE?
Kuna Mchungaji mmoja alituambia kwamba ulevi ni ugonjwa kama yalivyo magonjwa mengine.na matibabu yapo.......akaamua kutusaidia.
Akatufafanulia kwamba ugonjwa huu ni wa kiroho,kwa hiyo dawa yake ni 'spiritual healing'....
Basi akaamua kukaa nae na ndipo uponyaji ulivyo patikana toka mwaka 1999 wakati wa maombolezo ya Mwl.Nyerere mpaka Leo hii jamaa hayagusa kabisa,na mambo yake ni mazuri.