Pre GE2025 Kafara ya kushinda Uchaguzi huu ni kuteka na kuua watoto wadogo?

Pre GE2025 Kafara ya kushinda Uchaguzi huu ni kuteka na kuua watoto wadogo?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Komeo Lachuma

JF-Expert Member
Joined
Oct 31, 2014
Posts
7,926
Reaction score
17,030
Imani za kishirikina zimekuwepo sana kwenye chaguzi zetu kuu. Sana.

Huu ni mwaka uelekeo wa uchaguzi Mkuu 2025. Kumekuwa na wimbi kubwa la watoto kuibwa na kuuawa. Mara nyingi sana tunasoma habari hizo.

Rais anasema ni drama. Imenishtua. Hasemi kuwa polisi wafanyie kazi hizo "tetesi" ikiwa si kweli. Anasema ni drama yaani ame conclude kuwa si kitu zipuuzwe. Tukifikia hatua ya kupuuza masuala yanayohusua watoto basi tumefikia hatua ya mwisho.

Naaanza kuwaza. Je Rais anajua kinachoendelea mpaka haoni kama ni suala la kulikodolea macho makali? Atakuwa anajua. Maana yeye hujua kila kitu.

Chaguzi zetu zina imani za kishirikina sana. Si kidogo. Hali ni mbaya wengi watakuambieni haya nayosema. Ushirikina upo kwa asilimia 80 katika siasa zetu. Na kafara zipo sana tu kulingana na ukubwa wa jambo husika.

Tukemee hali hii tusiache hili suala lipite tu juu juu.
 
Back
Top Bottom