SoC02 Kafara zitatuinua kiuchumi?

SoC02 Kafara zitatuinua kiuchumi?

Stories of Change - 2022 Competition

Japhet Joseph

New Member
Joined
Sep 2, 2022
Posts
4
Reaction score
2
JE! KAFARA YA AINA YOYOTE INAWEZA KUKUINUA KIUCHUMI?.

Kumekuwepo na upotoshwaji wa kimila kwa baadhi ya makabila katika dhana halisi ya TAMADUNI za kiimani haswa imani za kishirikina, ambazo mpaka sasa zimeonekana kukatisha maisha ya watu. Imani hizi zimechukua taswira mpya inayokinzana na sheria za nchi pamoja na za kidini.

Imani hizi zimepelekea baadhi ya watu kujichukulia maamuzi yenye kudhoofisha maisha na uhalisia wa namna ya kuishi katika mazingira yetu. Kwa mfano waganga wa kienyeji wamekuwa ndio chanzo kikubwa cha udanganyifu hasa wanapofuatwa na wateja wao kwa lengo la kuagulia. Moja ya matukio kama haya yametokea mikoa ya Tabora, Geitq, na hata Iringa pia.

Kafara za damu au ubakaji zimechukua asilimia kadhaa mpaka sasa kiasi kwamba watoto ndugu na hata Wadogo zetu pengine wamelawitiwa na baadhi ya wanaume wanaokuwa na lengo la kutajirika kwa kwa kufuata mashariti ya waganga wao. Je! Wananchi tufanye nini kutoa hili tatizo? Serikali wanatusaidiaje kupambana na hawa watu??

PAZA SAUTI YAKO PIA
 
Upvote 1
Kafara ni kitendo au mkataba usio kuwa na warranty, tuchunge sana...!!
 
Back
Top Bottom