and 300
JF-Expert Member
- Jun 27, 2012
- 26,398
- 36,406
Leo nilienda Uchumi Supermarket pale Quality Plaza baada ya manunuzi kadhaa nikaamua nipate chakula cha mchana pale pale ndani kwenye Canteen/cafeteria yao..nikaagiza ugali kuku na mwenzangu akaagiza ugali beef tukaletewa duuh! kwanza nyama zilikuwa zinanuka kwa harufu mbaya na zikisindikizwa na jeshi la nzi na tuliporudisha kwa wahusika wakadai hawakubali kurudishiwa chakula baada ya kuuza ingawa hatukukigusa. tulianzisha tafrani mpaka tukarudishiwa pesa yetu. UCHUMI SUPERMARKET mmechemsha. huduma mbovu, customer service za ajabu zaidi wahudumu wenu wanaojidai ku-pack mizigo ya wateja wanaficha chini ya mifuko pale counter baadhi ya bidhaa za wateja na ikitokea mteja hajashtukia ndo imetoka hiyo. mimi walibana/walificha SET YA VISU, LOTIONS chupa 3. msipojirekebisha mtakimbiwa na wateja wote