Kafiwa au kafiliwa?

Kafiwa au kafiliwa?

Crucifix

JF-Expert Member
Joined
Feb 20, 2011
Posts
1,655
Reaction score
592
Nimekutana na hili neno kufiliwa katika gazeti moja la Kiswahili. Sasa nini neno sahihi, mtu kafiwa au mtu kafiliwa?
 
Yote ni sawa lakini kama utayatumia eneo mwafaka. Ukiwa kule Unguja wanasema 'kafiliwa', kwa mujibu wa lahaja yao, lakini kwa bara ni kafiwa! kufiliwa du! hutaeleweka na ukitamka kwa wakwe utanyang'anywa mke kwa utovu wa nidhamu.
 
Kaka upo sahihi kabisa na naamini mlengwa ameelewa barabara
 
Si ndio maana kukawa na jukwaa ili yajibiwe, ama?
Nakubaliana nawe, lakini mara ya kwanza niliposoma swali haraka haraka nilipatwa na mshtuko hapo kwenye "kafiwa, kafiliwa" Mawazoni nilikuwa nimeshaona kuna "r" katika hayo maneno hadi niliposoma mara ya pili kwa utulivu na kujuwa kumbe nimekurupuka!!!
 
Back
Top Bottom