Yote ni sawa lakini kama utayatumia eneo mwafaka. Ukiwa kule Unguja wanasema 'kafiliwa', kwa mujibu wa lahaja yao, lakini kwa bara ni kafiwa! kufiliwa du! hutaeleweka na ukitamka kwa wakwe utanyang'anywa mke kwa utovu wa nidhamu.
Nakubaliana nawe, lakini mara ya kwanza niliposoma swali haraka haraka nilipatwa na mshtuko hapo kwenye "kafiwa, kafiliwa" Mawazoni nilikuwa nimeshaona kuna "r" katika hayo maneno hadi niliposoma mara ya pili kwa utulivu na kujuwa kumbe nimekurupuka!!!Si ndio maana kukawa na jukwaa ili yajibiwe, ama?