kmbwembwe
JF-Expert Member
- Aug 16, 2012
- 10,892
- 7,780
Kama Kafulila na PPP yake hana shaka na Adani kama tulivyosoma mitandaoni basi ajue wananchi wengi taarifa za kushitakiwa hao watu kwa kupewa kandarasi marekani kwa kutoa rushwa zinathibitisha yale wamekua na mashaka nayo. Kwamba nchi wala haihitaji huduma kama za Adani.
Ni huduma za kudumaza nchi kujenga uwezo wa kujitegemea na kwa uhakika ni kukandamiza uwezo ambao upo nchini kutokana na vishawishi vya makampuni ya kinyonyaji kama haya ya kina Adani. Mtu kama Adani anatajirika kupindukia kwa muda mfupi kwa ulaghai kujifanya anawekeza kwenye uwekezaji za umma kwenye nchi kama Tanzania. Halafu wala hawekezi kitu.
Kwa kushirikiana na vigogo anaowahonga wanatoa taarifa na blaablaa kuhusu ufanisi ambao kwa uhakika ungeweza kufikiwa hata bila uwekezaji za kina Adani, DP world etc, kwa serikali kutumia tu uwezo ambao upo serikali.
Tungetarajia Adani kutoshwa kama ilivyofanyika Kenya. Tujitazame kwa makini nchi zetu tuache ujinga. Wananchi sasa wanaelewa vizuri kinachoendelea. Serikali yetu lazima iwe na uwezo kusimamia mashirika yake. Kuna watu wenye uwezo mkubwa tu ila kiongozi mkuu wa nchi anakuja na falsafa za kulea upigaji tu. Hapo ndio tatizo.