Mtumishiwetu
Senior Member
- Jul 13, 2022
- 196
- 346
Kwa muda mfupi ambacho Kafulila ameongoza Mkoa wa Simiyu tumeshuhudia mageuzi makubwa ikiwemo kumtaka Mkandarasi aliyejenga barabara ya Maswa- Mwigumbi chini ya kiwango kuirudia kwa gharama zake jambo ambalo watangulizi wake hawakuliona kama ni tatizo.
Kafulila amesimamia nidhamu ya ukusanyaji wa mapato kwenye Halmashauri za Mkoa wa Simiyu na kuondoa yale mazoea ya kuzigeuza halmashauri shamba la bibi fedha zinaliwa na watu wachache leo Halmashauri zote zimepaa makusanyo yake ndani ya muda mfupi wa uongozi wake na fedha nyingi zinakwenda kwenye miradi ya maendeleo ya wananchi.
Sijui watangulizi wake kwanini hawakusimamia hayo, leo tunaona Kafulila anafanya ziara kwenda kwenye vijiji kukagua shughuli za maendeleo na kusikiliza na kutatua kero za wananchi jambo ambalo wananchi walizoea kuwaona viongozi wa Mkoa kwenye matukio ya ziara za viongozi wa kitaifa Waziri Mkuu, Makamu wa Rais au Rais.
Kuna wahuni wameanza kujitokeza humu kumkatisha tamaa Kafulila kwa mwendelezo uleule wa kutaka akae tu ofisini asishughulike na matatizo ya wananchi na kusimamia makusanyo ya fedha za Serikali