Nimekutana na hii Clip ya Kafulila sijui ni ya lini na alikuwa katika tukio gani sifahamu ila nimevutiwa na hekima za hotuba yenyewe.
Katika video hii Kafulila anasema hapa duniani tuna kizazi bora zaidi kilichopo kaburini kuliko hiki kinachoishi duniani leo.
Ukisikiliza vizuri hiyo Clip Kafulila anasema, Leo tuna kizazi ambacho wazee wanahitaji kuwezeshwa kwa sababu ya uzee wao kwani wameishiwa nguvu.
Leo wanawake nao wanahitaji kuwezeshwa kwa sababu wao ni wanawake na mbaya zaidi vijana ambao ndio nguvu kazi ya Taifa nao wanahitaji kuwezeshwa kwa sababu wao ni vijana.
Kafulila anahoji, Kipo wapi kizazi kile ambacho kijana alichukua panga, shoka na jembe ili kuukabili msitu kujitajirisha na ikiwa Serikali itakuja itamkuta ametangulia shambani?
Kafulila anashanga leo kuna majengo ya Serikali maeneo mbali mbali yalijengwa miaka ya 1960 hata kabla ya Uhuru au miaka ya 1970 wakati wahandisi wa ujenzi wakiwa wachache kabisa.
Kafulila anashanga zaidi majengo hayo ya zamani kabisa leo yanapakwa rangi tu ili kusafisha kuta lakini leo majengo mengi ya madarasa na majengo mbalimbali ya Serikali yanayojengwa na Watanzania wenyewe hayadumu.
Leo, majengo mengi baada ya miaka mitano au kumi tu yanakuwa yamejaa nyufa Kila sehemu wakati leo ndio wakati ambao wahandisi wa Kitanzania wa Ujenzi wamejaa nchini"
Huenda ni kweli kizazi kilichopo kaburini kiliipenda zaidi Tanzania kuliko kizazi hiki tunachoishi kwani ni kizazi kinachotanguliza masilahi yao zaidi kuliko masilahi ya Taifa.
FIKIRI, LEO JENGO LA MWAKA 1960 HALINA NYUFA ILA JENGO LA MWAKA 2000 LIMEJAA NYUFA TUJITAKARI KAMA TAIFA.