Mwananchi Huru
JF-Expert Member
- Nov 20, 2021
- 2,128
- 1,896
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo Cha Ubia nchini Tanzania PPPC Bw. David Kafulila amekaririwa akisema kuwa nia ya PPP ni kuvuta na kuvutia mitaji , Ufanisi pamoja na Teknolojia toka Sekta binafsi Popote Duniani.
Mkurugenzi huyo ametolea mfano faida za moja kwa moja za PPP nchini Tanzania ilizoanza kuzipata toka kwenye Vivuko vya Bakresa pamoja na Ufanisi wa kihistoria uliofikiwa na DP WORLD kwani kwa kipindi kifupi DP WORLD imetoa matokeo ambayo hayajawahi kufikiwa kwa miongo mingi iliyopita.
Kafulila anaendelea kwa kusema Serikali inaleta sekta binafsi kwaajili ya kuvuta teknolojia Kwakuwa Sekta binafsi ndio yenye teknolojia bora zaidi kuliko ile iliyoko Serikalini na huu ni utafiti kwa Dunia nzima.
Anaendelea kwa kusema, zile pesa za walipa Kodi ambazo Serikali ingeipatia TEMESA ili kununua Vivuko Sasa pesa hizo zitaelekezwa moja kwa moja kwenye Ujenzi wa miradi mingine muhimu kama vile shule, Zahati au vituo vya afya Kwakuwa Sasa huduma za Vivuko zinatolewa na Bakhresa kwa utaratibu wa Ubia na Serikali bila kutumia Senti moja ya Kodi Wala Mkopo wowote.
Tumia muda wako kupata madini toka kwa Kafulila.
===