Mjinga wewe kama hujui kwamba serikali ilienda kufanya marekebisho baadhi ya maeneo yaliyokua na utata umebakia kushupalia upumbavu!Niliwaambia waliokuwa wanapiga makelele ni wale waliokuwa wanavusha mizigo bila Kodi wao na washkaji zao Sasa upuuzi wa hivyo hamuwezi Ukuta private sector ikishika hatamu.
Yapi wewe boya? Si mnasema Samia ameuza Mali zenu nyie nyumbu?Mjinga wewe kama hujui kwamba serikali ilienda kufanya marekebisho baadhi ya maeneo yaliyokua na utata umebakia kushupalia upumbavu!
Hopeless hungry black skinWanatekeleza maono ya Rais Samia, private sector driven minded.
Ndio nini hii?Hopeless hungry black skin
Sio Kweli, fuatlilia vizuriKwenye bandari hata Mimi naungana na Kafulila
Palikuwa na urasimu sana pale ila Leo kwakweli acha Samia aongoze tu hata kama mpaka 2035 ni sawa tu
MKATABA MWINGINE BANDARINI NA MISRI WAZUA TAHARUKI YA CHINI KWA CHINI!
Ndugu Watanzania!
Tumepata taarifa kuwa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) na Chuo cha Arab Academy for Science Technology and Maritime Transport (AASTMT) cha Misri wametia sahihi makubaliano ya kushirikiana kutoa mafunzo ya shughuli za kibandari kwa Wafanyakazi.
Kwa mujibu wa taarifa hizo,makubaliano hayo, Tanzania kupitia TPA itapeleka watumishi wake kusoma Misri. Hii haitakuwa scholarships, bali Tanzania itakuwa ikilipia watu wake ada. Hata hivyo, makubaliano hayo yamezua mjadajala mzito miongoni mwa wadau ambao ni pamoja na manahodha wa meli, wahandisi wa meli na wahadhiri katika Chuo cha Ubaharia Tanzania yaanjli Dar es Salaam Maritime Institute (DMI) ambacho hutoa kozi hizo wakidai kuwa hiyo ni njia ya kukihujumu Chuo hicho. Baadhi ya hoja zao ni hizi:
Matumizi mabaya ya Fedha: Kutuma watumishi nje ya nchi kutagharimu fedha nyingi ambazo zingeweza kuwekezwa katika Chuo cha DMI ili kukiimarisha zaidi.
Kudhoofisha na kudhalilisha vyuo vya ndani: Hatua hiyo itaidhoofisha DMI na kufifisha zaidi ukuaji wake.
Kutelekeza Uchumi wa Blue: Kuimarisha vyuo vya ndani kunaiweka vizuri Tanzania katika kuinua rasilimali za Baharini.
Kukosekana kwa uwazi wa mchakato huo: Kwa kuwa mchakato huo haukuwa wa wazi, kuna maswali kuhusu kama uamuzi huo umebeba manufaa ya umma au una manufaa binafsi.
Wadau wanapendekeza kuwa:
TPA iwekeze zaidi katika Chuo chetu cha DMI kwa kuboresha na kuimarisha mitaala na kama itawezekana kuwaalika wakufunzi kutoka nje ya nchi ili kushusha gharama za Tanzania kupeleka watumishi wake nje. Njia nyingine ni kupeleka kusomesha wahadhiri kwa kozi ambazo hazipo nchini ili wakirudi waanzishe kozi hizo hapa Chuoni kwetu au pia kusomesha wahadhiri nje kwa kozi za PhD.
Wadau wanashangaa uamuzi wa TPA kupeleka vijana kusoma Uhandisi wa Meli nchini Misri wakati DMI ipo na inaheshimika sana hata nchi za Afrika Magharibi wanataka kuja kusoma DMI lakknky TPA wanaona Chuo hiki hakina maana.
Hata hivyo, kwa kuwa wadau hao wengi wao ni waajiriwa wa Serikali wanaogopa kujadiliana kwa uhuru na uwazi huku wengi wakitumiana ujumbe wa maandishi hata kupigiana simu.
Sisi Askofu Mwamakula tulipopata taarifa hizi kupitia kwa mmoja wa wastaafu tumeona ya kuwa ni vizuri tuweke hadharani jambo hili ili kuwapa uhuru wadau kuliweka andiko hili huko katika makundi yao sogozi.
Pamoja na hayo, kwa kuwa baadhi wamehoji juu ya uwazi wa mchakato huo makubaliano hayo, tunashauri mchakato huo uchunguzwe kama ulikidhi vigezo kwa mujibu wa Sheria za nchi yetu kuhusu masuala ya mikataba na nchi au taasisi za kimataifa. Je, kama wadau wakuu wanahoji makubaliano hayo, ni nani aliyeshiriki katika kushauri juu ya jambo hilo?
Je, kulikuwa na ushirikishwaji wowote? Ni nani alihusika kutoa ushauri wa kitaalamu kuhusu hili? Je, kuna shida gani ilijitokeza katika Chuo chetu cha DMI hadi tuingie mikataba ya kutaka kusomesha watumishi katika fani ambazo zipo DMI? Je, mkataba unaeleza ni fani gani na kwa ngazi gani za kusomesha watu kule Misri? Je, mkataba huo unatoa kipindi cha muda gani? Je, mkataba huo unaweza kuwekwa hadharani kwa wadau ili waweze kuusoma na kuuelewa?
Je, nini kimekushangaza? Je, nini maoni yako?
Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula
Dar es Salaam, 3 Februari 2025; saa 5:20 usiku
Huo sio mkataba wa Ubia ila ni makubaliano ya ufanyaji kaziMbona hapa unatisha watu bure
Kwenye bandari hata Mimi naungana na Kafulila
Palikuwa na urasimu sana pale ila Leo kwakweli acha Samia aongoze tu hata kama mpaka 2035 ni sawa tu
Ila Kafulila kazi anayoifanya ingekuwa yeye ni Waziri naamini angesukuma vitu vingi sana katika hiyo sektaMkurugenzi Mtendaji wa Kituo Cha Ubia nchini Tanzania PPPC Bw. David Kafulila amekaririwa akisema kuwa nia ya PPP ni kuvuta na kuvutia mitaji , Ufanisi pamoja na Teknolojia toka Sekta binafsi Popote Duniani.
Mkurugenzi huyo ametolea mfano faida za moja kwa moja Tanzania ilizoanza kuzipata toka kwenye Vivuko vya Bakresa pamoja na Ufanisi wa kihistoria uliofikiwa na DP WORLD kwani kwa kipindi kifupi DP WORLD imetoa matokeo ambayo hayajawahi kufikiwa kwa miongo mingi iliyopita.
Kafulila anaendelea kwa kusema Serikali inaleta sekta binafsi kwaajili ya kuvuta teknolojia Kwakuwa Sekta binafsi ndio yenye teknolojia bora kuliko ile iliyoko Serikalini na huu ni utafiti kwa Dunia nzima.
Anaendelea kwa kusema, zile pesa za walipa Kodi ambazo Serikali ingeipatia TEMESA ili kununua Vivuko Sasa pesa hizo zitaelekezwa kwenye Ujenzi wa miradi mingine muhimu kama vile shule, Zahati au vituo vya afya Kwakuwa Sasa huduma za Vivuko zinatolewa na Bakhresa kwa utaratibu wa Ubia na Serikali bila kutumia Senti moja ya Kodi Wala Mkopo.
Tumia muda wako kupata madini toka kwa Kafulila.
View attachment 3224842
===
Kwani yeye Nehemiah kapatikanaje?Maono ya Nehemia yatazaa matunda tu ikiwa nafasi za CEOs, wenyeviti wa Bodi na wajumbe wake watapatikana kwa njia ya ushindani, na si kupeana tu kwa teuzi.
Nafasi zitangazwe watu waombe, wafanyiwe rigorous interviews kupata competent people.
Short of that ni business as usual
Haina haja ya kutumia pesa ya Serikali wakati Kuna watu binafsi wako tayari kwa hiloHili la Bakhressa na vivuko vyake ni kushindwa kutimiza wajibu wake serikali, mwishowe mtaita Wachina waendeshe JWTZ
Huwezi kuwaona tenaWako wapi wale burukenge waliosema bandari imeuzwa?
Na bei imepanda au umeshu ka?Sasa hivi moja hadi mbili tu
Bei ya kawaida tu nijuavyo mimiNa bei imepanda au umeshu ka?
dhuluma ya nini exactly? port charges ni visenti tu, makusanyo makubwa yanakuwa ni TRA indirect, umeona makusanyo ya TRA yalivyoongezeka? assume hio figure ya 60/40 ni sawa, mapato TRA umepata trilioni 16, port charges 0.5-1 trilion kati ya hizo 200-400b inabaki dp world na 16.3T-16.6T inabaki serikalini huoni ni fair deal?..mgawanyo wa 60 / 40 kati ya Tz na Dp World nadhani dhuluma.
..tulihitaji ufanisi ktk bandari yetu lakini sio kwa kudhulumiwa kiasi hicho.
data zipo ila sio uzi huuAweke data sio maneno matupu, ngapi zinaingia hazina compare na kabla ya mkataba? ufanisi vipi siku ngapi kutoa mzigo na cost zimepungua au kuongezeka? Na mizigo kwa ujumla imeongezeka au? ….etc