Kafulila: Mzushi wa MCC na Escrow

singidadodoma

JF-Expert Member
Joined
Nov 11, 2013
Posts
4,394
Reaction score
1,536
Na Prince M. Bagenda

DAVID Kafulila ni Mbunge wa Kigoma Kusini kwatiketi ya chama cha NCCR-Mageuzi, siku zote amekuwa akikuza na kutoa taarifa zisizo sahihi juu ya kusitishwa misaada ya wahisani. Sasa ameingia mkenge kuhusu fedha za Millenium Challenge Corporation (MCC) ambazo alikuwa anadai zimezuiwa kwa sababu ya serikali kutochukua hatua za kuridhisha kuhusu watuhumiwa wa Escrow.

Ndani na nje ya Bunge Kafulila ameujengea umma imani kuwa kusitishwa kwa misaada ya wahisani kwa ujumla, ikiwemo na shirika hilo la Kimarekani la utoaji misaada (MCC) kumefanya uchumi wetu uyumbe mpaka shilingi ya Tanzania kuporomoka kwa kulinganisha na dola ya ki-Marekani. Kutokana na taarifa ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ambayo iliibua maswali mengi yanayohitaji majibu kuhusiana na madai kwamba fedha zilizokuwa zimetunzwa katika akaunti ya ESCROW Benki Kuu ya Tanzania ziliondoshwa kinyume cha utaratibu ambapo baadhi ya maofisa wa serikali inadaiwa walihongwa na wengine kupindisha taratibu katika zoezi la kuziondosha fedha hizo na pia kutokulipwa kwa kodi za serikali.

Kwa Kafulila suala hilo la kusitishwa au kukosa kwa mikopo ya nje limekuwa gumzo kwake. Badala ya kufikiri kwa makini jinsi gani nchi ifanye nini kujinusuru na hali hii ya kutengemea misaada ya nje, kwake imekuwa ndio kupaza sauti kucha kutwa.

Lakini ameumbuka kutokana na ziara ya ujumbe wa biashara kutoka Marekani ambao pia ulihusisha wajumbe kutoka MCC; iliweka wazi juu ya uongo huo mkubwa. Hakuna mahali popote katika taarifa yao iliyotolewa na wajumbe hao wa MCC palipotajwa kuwa akaunti ya Tegata Escrow ni chanzo kikuu au miongoni mwa sababu zilizosababisha MCC kushindwa kusaini mkataba au makubaliano ya mradi huo kwa awamu ya pili.

Kamran Khan (mwakilishi wa MCC aliyekuwa na Ujumbe wa Biashara kutoka Marekani) alisema, "wadau wote wawili-Serikali na MCC, wamejikita katika kutekeleza sera mpya ambazo wadau hawa wamekubaliana; ambazo ni kurekebisha muundo wa tozo na ushuru (tariff restructuring), sera, lakini pia taratibu za kisheria zinazoratibu sekta ya gesi."

Huku akitoa matarajio ya kusaini kwa awamu ya pili ya mradi wa MCC kwa niaba ya ‘USA Trade Mission' Bwana Khan anasema kuwa, " makubaliano ya awali ya Tanzania yalikuwa muhimu. Hasa hasa yalilenga katika sekta ya uchukuzi na nishati kama mihimili muhimu ya kukuza uchumi wa nchi."

Mkataba wa pili wa MCC (MCC-2) kwa Tanzania utagharimu zaidi ya dola za kimarekani milioni 700 ( sawa na trilioni 1.5). Mradi huo wa pili utajikita kwa kiasi kikubwa katika sekta ya umeme, ikiwemo ni pamoja na uwekezaji katika miundombinu hali kadhalika sera; pamoja na kuziunda upya mamlaka za urekebu na taasisi zake (regulatory and institutional reforms). Pengine hii ni kutokana na funzo walilolipata kutokana na utekelezaji wa MCC-1.

Mradi wa makubaliano ya MCC-1 ulitekelezwa Tanzania Bara na Zanzibar kuanzia mwaka 2008 hadi 2015 huku zaidi ya dola za kimarekani milioni 698 (trilioni 1) zikiwa zimetumika katika miradi ya maji, barabara na nishati ya umeme. Hata sehemu kubwa ya mpango wa umeme vijijni umekuwa ukifadhiliwa na MCC-1.

Kafulila alikuwa mwepesi wa kukurupukia suala hili na kulieneza kwa umma kuwa wahisani wamesitisha misaada kwa sababu ya sakata la uchotwaji pesa kutoka Akaunti ya Tegeta Escrow. Akiwa kama mbunge, labda Kafulila anafahamu fika kwamba wahisani hawakutoa fedha walizoahidi za kukamilisha bajeti. Na mara nyingi fedha walizoahidi, hata wakizitoa huwa siyo kiasi chote kilichoahidiwa.Ikumbukwe kuwa maeneo makubwa ya makubaliano mapya kati ya Serikali ya Tanzania na MCC yanajumuisha sekta ya umeme, ikiwemo uwekezaji wa miundombinu, hali kadhalika sera na kuboresha taasisi za urekebu.

MCC, ukipenda iite Kampuni ya kutoa misaada, imekuwa ikishirikiana na serikali katika uwekezaji wa nishati na miundombinu. Tunaweza kujifunza nini kutokana na hili? Nishati na Miundombinu ni sekta muhimu katika ukuaji wa uchumi.
Serikali ya Marekani ambayo imeanzisha mradi wa ‘Power Africa' na pia mpango wake wa kudhamini kampuni hizi katika kuwekeza kwenye uzalishaji wa umeme na ujenzi wa miundombinu hasa reli, ni dhahiri kwamba mazingira ya uwekezaji yameandaliwa. Swali ni kwamba, ni biashara ipi inakubalika na kwa mazingira yapi?

Uzoefu unaonesha kwamba mazingira ambayo wahisani wanayahitaji ni yale ya makampuni ya kimataifa yenye ujuzi na utaalamu mkubwa, yaweze kuwekeza lakini pia waweze kufilisi mitaji na uwezo wa kibenki katika kuhamisha faida zao. Lakini pia kuwepo kwa mikataba yenye makubaliano ya unyonyaji na uwezo wa kumiliki maliasili yetu. Wawekezaji wa ndani ambao ni washikadau (wanahisa) wadogo, wao hufanya kazi ya uendelezaji wa miradi na baada ya hapo wanakaimishwa au kukasimu kazi za uendelezaji wa mradi na wala si zaidi wala pungufu ya hapo. Gumzo la haya huja kwa mazingira yetu kuwa katika unyonyaji wa maliasili na kudunisha uchumi au kuboresha huwa kuna uhusiano wa kisiasa ambapo wanasiasa kwa nadra huyafanya hayo katika kulinda nafasi zao za kisiasa. Huko ni kujikawiza tu kwa kitu usichokijua.

Pengine kwa hatua hii twaweza kumuuliza Kafulila na wabunge wengine kuwa pamoja na kutoa jasho jingi katika kumkamata mwizi wa fedha za akaunti ya Tegeta Escrow, EPA na Richmond, ni kwa kiwango gani Bunge limejisumbua kutafuta taarifa na kutaka kujua kuhusu muundo na matatizo ya taasisi ambayo hutoa tahadhari kuhusu ubadhilifu wa mali ya umma?

Pili, ni kwa kiasi gani wawekezaji wa ndani ambao ni washikadau (wanahisa) wadogo kwenye miradi mikubwa wamejikinga dhidi ya wawekezaji wakubwa juu ya ukiukwaji wa sheria za makampuni, ukaguzi na usimamizi wa fedha kwa faida ya wanahisa hao wadogo?

David Kafulila amekuwa mlafi wa kutaka kujipatia umaarufu. Mwanasiasa huyo ambaye anatoa umuhimu mkubwa kwa UKAWA bila kuiacha NCCR-Mageuzi-chama kikuu kikongwe cha upinzani ambacho nami nilikuwako huko, Ukawa ambayo baadhi ya wanasiasa wanaitanguliza wakati hawaiwekei misingi ambayo inatokana na yale ambayo vyama ndani ya Ukawa vilikwisha kuweka misingi nikiunga mkono jitihada za kuja kupata taifa. Watu hufikiri ni vigumu kuachana na chama chako kidogo cha zamani ambavyo mara chache huwekwa kwenye vyombo vya habari kama rejea na bingo kwao.

Kwa kuyatazama haya katika mtazamo binafsi zaidi, Kafulila amejikuta yupo peke yake katika adhima yake ya kuinanga Serikali. Katika mtazamo binafsi ameituhumu serikali kwa kubana na kupunguza makali ya maamuzi ya Bunge ya Novemba 2014 juu ya maafisa na watumishi waliohusika na uchotwaji wa fedha za akaunti ya Tegeta Escrow.

Pamoja na hila za kuwaweka wazi hao wanaowaita mafisadi na jitihada za kutaka kuwanyonga kutokana na Escrow hiyo imekuwa tena si kipimo sahihi katika medani za kisiasa za sasa. Jamii na wanasiasa sasa wamegundua juu ya upotoshwaji mkubwa uliotokana na taarifa ya kamati ya Bunge ya Hesabu za Umma (PAC) kuhusu akaunti ya Tegeta Escrow.

Tayari uchambuzi wa kina umefanywa na Salim Khatri unaonesha wazi kuhusu uongo huo wa taarifa zisizo sahihi bungeni. Tunaweza kubainisha kwamba Bunge lilipotoshwa. Lakini pia kwa kuchambua nini msimamo wa Kafulila bungeni, nimegundua kuwa Bunge si mahali sahihi kwa vijana wadogo wanaoongozwa na itikadi za kuivamia dunia kwa mitazamo ya uhuru, udugu, usawa na haki kwa wote. Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Anna Makinda alipokuwa anaongoza mijadala kuhusu Tegeta Escrow, bungeni alitoa tahadhari kwa wabunge kuwa makini na wajitenge na rushwa kwani wengi wao wataishia jela.

Lakini habari ya Tegeta Escrow ni wazi haitajifia hivihivi David Kafulila sio mwanzilishi wa sakata hili la Escrow bali ni Zitto Kabwe. Lakini Kafulila alikuwa amtetee Zitto ambaye baadaye alifukuzwa na chama chake CHADEMA ambacho kilimtuhumu kwa usaliti na kushirikiana na chama tawala-CCM na pia Idara ya Usalama wa nchi. Zitto hakutaka suala hilo life kwani alikuwa amepewa nyaraka na maagizo na watu wengine alifanyie kazi. Kama rushwa ingelitumika wahusika walivyotaka, suala hilo lingezimwa. Halikuzimwa kutokana kwamba baadhi ya watu hawakupata mgao waliotaka.

Kafulila hakutaka kuonekana kama ni ‘mshabiki wa siasa za Zitto; ila alizidi kutoa tuhuma dhidi ya Waziri wa Nishati na Madini (Sospeter Muhongo) na kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG)-(Jaji Fredrick Werema) ambao kwake aliwaita wezi wa mchana. Huku AG akimjibu kwa kumuita Kafulila ‘tumbili', mnyama mdogo anayependa sana kula ndizi na ambaye inasemekana kuwa sisi binadamu tumetokana na mnyama huyo.

Makubaliano ya MCC na Tanzania kuhusu kutoa misaada kwa miradi mipya inaweza kuwa hatari na ya gharama kwa uchumi wa nchi yetu kwa siku za usoni. Kitu ambacho Kafulila na wengine wengi hawajisumbui kufikiria juu ya hili labda kwa sababu inahitaji ufikiri wa hali ya juu.

Hata kabla ya taarifa hizo za MCC ofisi za Utumishi wa umma imewasafisha baadhi ya watumishi waliohusishwa na sakata la Escrow. Awali walichunguzwa kwa tuhuma za kukosa maadili.

Pia Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeyahamisha mashauri yote ya rushwa yatokanayo na tuhuma za kunufaika na fedha za Akaunti ya Tegeta Escrow yanayowahusu watumishi wa umma kwenda Mahakama Kuu, sababu ya kuhamisha kesi hizo ni madai ya wahuska kwamba kulikuwa na ukiukwaji wa sheria na Katiba namna Bunge lilivyoshughulikia masuala ya Tegeta Escrow wakati huo huo shauri likiwa mahakamani.

Kwa hali inayojitokeza haya yote, ni suala la muda tu, kwamba maamuzi ya Bunge la Novemba 2014 kuhusu akaunti yaTegeta Escrow hayatoheshimiwa tena.

chanzo taifa imara
 
Huyu huyu David?
 
Huyu Kafulila alikuaga Anafulila kweli kweli (in Magu voice)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…