Jabali la Siasa
JF-Expert Member
- Jul 10, 2020
- 2,823
- 2,466
Hiki ndicho alichoandika Director wa PPP Tanzania Bw. David Kafulila huko kwenye akaunti yake ya X zamani tweeter.
Mkurugenzi huyo ameandika haya ili kuwatoa hofu wanaodhani huenda nchi yetu ikapata hasara ya mali na fedha kwa kuingia Ubia na Sekta binafsi toka ndani au nje ya Tanzania.
KAFULILA anarejelea Serikali ya awamu ya tatu Chini ya Hayati Rais Dkt. Benjamin Mkapa ambae katika kitabu chake Cha "My Life My Purpose " anasema baada ya kuuza mali za Umma kwa ubinafsishaji yakiwemo mashirika makubwa kama NBC kwa kupitia PSRC yaani Parastatal Sector Reform Commission anakiri alifanya makosa kuifuta tume hiyo ili ifanye ufuatiliaji wa mali zake zote ilizozifanyia ubinafshaji jambo lililozaa watu kuchukua mali za umma na kuzibadilishia matumizi, kukopea benki na uharibifu mwingine mwingi.
Kafulila anasema kwenye PPP Serikali na Sekta binafsi watamiliki mradi kwa pamoja na Serikali itakuwa ndio mwangalizi mkuu wa mradi kwa muda wote wa Mkataba na hii ndio tofauti kati ya Ubinafsishaji wa kipindi cha awamu ya tatu na Ubinafsishaji huu wa awamu ya sita kwa njia salama ya PPP.
Kafulila anasema PPP haiuzi mali za umma kama ilivyokuwa kwa PSRC bali inakodisha kwa kipindi maalum na baada kukodisha Serikali haiondoki kwenye mradi kwa kipindi chote cha Mkataba.
Na kwa ile miradi mipya itakayojengwa kwa Ubia kama zile Hosteli pale CBE baada ya muda wa Ubia kuisha miradi ile inarudi kuwa mali ya Serikali kwa asilimia 100.
Hata hivyo, ingawa haimaanishi Ubinafsishaji wa awamu ya tatu lilikuwa ni jambo baya hapana kwani ilikuwa ni njia sahihi ya kujenga Uchumi wa kisasa "modern economy" lakini matatizo hayawezi kuisha kabisa ila uamuzi wa Mzee Benjamin Mkapa wa ubinafshaji umekuwa na faida nyingi kuliko hasara Leo.
Pia soma Kwani Tulifeli vipi kwenye Ubinafsishaji wa Awamu ya 2 hadi Tufaulu sasa kwenye PPP ya David Kafulila?
Hivi PPP ya David Kafulila inafika hadi Zanzibar Kwenye Visiwa walivyopewa Wawekezaji?
Nauliza tu Ili kupata ufahamu kama Ofisi ya David Kafulila inatenda kazi zake hadi Zanzibar Nimeona kule Zanzibar PPP inafanya Vizuri Visiwa vilivyokuwa mapori Sasa vinaboreshwa kiuwekezaji Nawatakia Sabato njema 😃
Why Mkapa pushed through privatisation despite criticism
When one thinks of the privatisation policy in Tanzania, the name of President Benjamin Mkapa—who died on Friday—comes into mind at the top.