Kafulila umejijengea kaheshima flani hivi, nakushauri acha ku comment kila kitu

Pantosha

JF-Expert Member
Joined
Sep 22, 2022
Posts
640
Reaction score
958
Hivi karibuni nikekuwa nikimuona mdogo wangu Kafulila akitoa maoni yake kwenye kila kitu uenda ni kutokana na nafasi yake ya Ex. Director wa PPPC ndiyo maana anakuwa na munkari ya kuongea sana. Ila hekima ni pale unapotulia na kutoa ufafanuzi wenye busara na logic.

Suala la serikali kununua umeme kutoka Ethiopia linajitaji ufafanuzi wa kina kabisa na serikali ije na logical reasons za kufanya hivyo. Kwamba imeshindikana nini kwa serikali kuzalisha umeme kwa bei nafuu, kuzuia upotevu wa umeme wakati wa usambazaji, kwa nini Ethiopia waweze sisi tusiweze, na kwa nini tuendelee kuzalisha umeme kwa gharama kubwa na wakati kuna options za kununua kwa gharama kubwa, tumekipangaje ikitokea Ethiopia wakasema hatuwauzii umeme hadi mtekeleze 1,2,3? Tumeshuhudia huduma zikisitishwa pale diplomasia inapo shake kidogo.
Mfano: TZ na Kenya: Msiuze mahindi kenya
Russia na EU: Kata usambazaji wa gesi EU
Marekani na Canada: Hakuna uingizaji wa maziwa, nk.

Msiwe wavivu wa kutafuta solution za kujitegemea.
 
Mlizoea kumnanga mama na watu wako kimya Sasa naona Kafulila Yuko pampa to pampa😂😂
 
Tumbili hajui ana maadui wengi huko CCM kuliko anavyofikiri wanamlia timing tu atajaa kwenye 18 zao, asijesema hakuambiwa.
 
Ni tapeli wa mali za umma, hivyo lazima asifie ili awe salama
Mzee wa kuleta statistics na akatupia kiingereza kidogo basi sisi watanzania tushasema ni hazina kwa taifa. Watanzania huwa tunasema kiingereza kwani kitu gani, ila baada ya yule mtoto wa shule ya tanga kuzungumza kiingereza tukasema angekuwa mkubwa alipaswa kupewa hata uwaziri, sijui hoja ya kiingereza ni kitu gani hapa ilipoteaje.
Abby Chams watanzania wanamwona ni msanii mwenye akili sana kisa anajua kuzungumza kiingereza basi ni genius. Vigezo vya kuwa hazina ya taifa tanzania ni vya kipekee dunia nzima. Sometimes vinahusisha kuvaa scarf na tai za bendera ya taifa au kutumia neno uzalendo kila mara.
 
Moja ya sifa kuu ya Tumbili ni Udanganyifu na kulaghai, tumbili wanaweza kutumia ulaghai au udanganyifu kupata chakula au rasilimali nyingine. Hii inaweza kuonekana kama unafiki, lakini kwao ni njia ya kuishi.
 
Tunaowapa dhamana ni wavivu wa kufikiri wanajulisha mwisho kabisa badala ya kupata mawazo kama ya kwako kabla ya mradi
 
Maadui hata Wewe unao, nyie CHADEMA mnajifanya mnahekima sana, Jibuni hoja za Kafulila
Mimi nimetoa tahadhari tu wala sina ugomvi na Kafulila, na niliyoandika nimeandika.
 
Moja ya sifa kuu ya Tumbili ni Udanganyifu na kulaghai, tumbili wanaweza kutumia ulaghai au udanganyifu kupata chakula au rasilimali nyingine. Hii inaweza kuonekana kama unafiki, lakini kwao ni njia ya kuishi.
Chukua chako mapema, CCM
 
Aache kukomenti kila kitu ili atumbuliwe?. Angetaka kujilindia heshima yake angekataa hicho cheo mapema kabisa!. Kachagua cheo ili apoteze Heshima yake!. Kupata vyote kwenye hayo mazingira haiwezekani.
 

hilo ni liCHAWA tu, hamna kitu cha zaidi
 
System imejaa matapeli tupu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…