Kagame alikua na mkono kwenye mauaji ya Thomas Sankara?

kimsboy

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2016
Posts
9,846
Reaction score
20,319
Kwenye pita pita mbalimbali nimekutana na maelezo kuwa kagame alikua na mkono kwenye mauaji ya rais wa zamani wa Burkina faso Bwana Thomas sankara

Kwa mliomjua kumsikia na kujuwa sankara alikua mzalendo wa kweli aliyeibadilisha nchi yake kimaendeleo muda mfupi tu na kuleta maendeleo makubwa lakini akaja kuuawa

Hakuna kifo cha mzalendo mweusi ambacho moyo wangu umekua ukiulilia kama wa huyu thomas sankara

Nilivyokutana na hii clip ya global tv huko youtube inayozungumzia huyu mzalendo hakika lazima machozi yakulenge[emoji1313][emoji1313]

Nimesikia kagame alihusika 100% kwa tetesi zilizopo yaani kama ni kweli basi kagame mwisho wake utakua mbaya na anguko baya sana
 
Duh! Simpendi kagame ila kwa hili mtakuwa mnamuonea, sankara aliuliwa na rafiki yake wa tokea utotoni kwa tamaa ya madaraka
Nasikia alikua kwenye hilo genge la mauaji
 

Burkina Faso na Rwanda wapi wapi wakati hata Kijiografia tu ziko mbali mno. Siku zingine hakikisheni mnapokuja Kuanzisha Mada hapa basi Vichwani mwenu ama Gongo au Bangi mlizotumia ziwe hazijawazidi Kipimo. Kuna Watu wengine huwa mnajidhalilisha na kuonyesha waziwazi jinsi mlivyo Watupu Vichwani.

Kwa kukusaidia tu hasa kwa nchi za Afrika zetu hizi Mipango mingi ya Kimapinduzi hufanywa na Watu ama walio ndani au walio nje ya nchi husika ila iliyo na ukaribu wa Kijiografia lakini ni ngumu leo hii Rais au Mwana Mapinduzi wa Botswana akasababisha Machafuko / Mapigano nchini Chad.

Vitu vingine wala havihitaji Akili Kubwa kuvijua ila najua dhamira yako Kuu hapa ni Kumdhalilisha na Kuzidi Kuonyesha na Kuwaaminisha Wana JamiiForums kuwa Rais wa Rwanda Paul Kagame ni Mtu mbaya sana wakati hata hapa nchini Kwako una Watu / Viongozi pengine wabaya na makatili kuliko huyo Kagame. Na najua wapo Watu watakuamini kwa haya Madai yako japo najua baadhi wenye Akili timamu na zilizotukuka watakupuuza tu.

Sijui ni Mtanzania gani aliyewapeni Sumu hii Kali Watanzania ya Kumchukia hivi Rais wa Rwanda Paul Kagame na Wanyarwanda wote hasa hasa wa Kabila la Watutsi ( Tutsi ) wakati hakuna nchi na Watu wanaowapenda Watanzania na Kuwaheshimu kama Rwanda na Wanyarwanda. Na leo niwahakikishieni tu kuwa Rais Paul Kagame hayuko hivyo kama ambavyo Watanzania wengi ( siyo Wote ) mmelishwa ' Propaganda ' mbaya dhidi yake ambayo mmeiendeleza hadi kwa Wanyarwanda wenyewe. Watanzania mnapendwa na kuheshimiwa sana na Wanyarwanda kuliko ambavyo mnajua.
 
Hao unaowatetea
Kwa taarifa yako ni kwamba wamelaaniwa
Waliuana wao kwa wao kwa mambo ya kijinga sana

Huwezi kumchinja ndugu yako au jirani yako alafu Mungu akakuacha salama hawana upendo wowote kwetu hivi kweli walishndwa kupendana wao kwa wao waje kukupenda wewe mchoma MKAA mmatumbi wa huko kyambankumbe

Achana nao hao hata kama hakuhusika achana nao wamelaaniwa wao na vizazi vyao
 
blaise compaole killed Sankara

 
Hata historia ya Patrice Lumumba na kifo chake inahuzunisha sana!

Ni mzalendo wa kweli na mtu mweusi halisi!
 

Tafuta Kitabu cha The Rwanda Crisis kilichoandikwa na Bwana Gerald Prunier kisha utagundua ni akina nani ' exactly ' kati ya Watutsi na Wahutu ndiyo walichinja Wenzao vibaya na wanastahili kabisa Laana ya Mwenyezi Mungu. Siku zingine jitahidi Kwanza kwanza uwe na ' Intellectual Facts and Data ' juu ya Jambo ambalo labda huna uhakika nalo kuliko Kukurupuka hivi kama Mgonjwa wa Akili / Mwendawazimu.
 
Wanaomchukia kagame ni bavicha, kwa sababu ya urafiki wake na magu! Hawana jipya
 
USITUTOE KWENYE RAMANI
NSGAYI ANALIAIBISHA TAIFA
 
Tatizo humu kuna watu wajuaji sana hata kuchangia inakuwa kama ni tatizo.
Lazima ukubali kile wao wanajua au kutaka!
Nyandu tupu!
 
Je, kwanini wengi wenu humu hamjui kuandika swahili kwa usahihi kwenye thread title zenu?

Sisi tunaojifunza kiswahili humu pia.. mnatuboa.. na hapo nimepatia au?
 
Hili sasa ndo linaitwa povu
 
Si ungefanya tu hata research kidogo ndugu? Mwaka 1987 Kagame alikuwa na umri gan na alikuwa na nguvu gani za kimamlaka kumpindua na kumwua Sankara, na kwa maslahi yepi hasa maana Burkina Faso siyo nchi jirani na Rwanda wala Uganda alipokuwa akiishi Kagame wakati huo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…