Zanzibar-ASP
JF-Expert Member
- Nov 28, 2013
- 12,151
- 44,120
Nini?2. Kuwekewa vikwazo vya kiuchumi (Hata hii Tanzanite anayoivuna hapa Tanzania kwa wingi anaweza kukosa pa kuiuza)
Wewe fahamu tu, japokuwa madini ya Tanzanite yanachimbwa hapa Tanzania pekee, lakini kwenye kuuza Tanzanite soko la dunia, Tanzania imekuwa ikishindana na India (ambaye ndio anaongoza), Vietnam, Kenya, Rwanda nk. Hapo hapo mnunuzi mkuu akiwa USA.Nini?
Asante kwa ufafanuzi.Wewe fahamu tu, japokuwa madini ya Tanzanite yanachimbwa hapa Tanzania pekee, lakini kwenye kuuza Tanzanite soko la dunia, Tanzania imekuwa ikishindana na India (ambaye ndio anaongoza), Vietnam, Kenya, Rwanda nk. Hapo hapo mnunuzi mkuu akiwa USA.
Umejisikia vizuri baada ya kuandika lugha ya mkoloniWithin the realms of what goes around resides the magnitude and severity of what comes around.
Sidhani kama kutimuliana maofisa wa kibalozi kati ya Rwanda na Ubelgiji ni kwamba Rwanda wametangaza vita.Kama kuna makosa ya Kidiplomasia ambayo Kagame amewahi kuyafanya basi kosa kubwa zaidi ni kitendo cha kutangaza kuvunja uhusiano wa Kidiplomasia na Belgium sasa. Huo ni mtego ambao ametengenezewa Kagame lakini akashindwa kuung'amua vyema labda kwa sababu ya kiburi, hasira na msongo wa mapambano.
Kwa muda sasa imeelezwa kuwa Belgium huenda ndio taifa kinara wa kunufaika na madini ya DRC kwa mgongo wa Rwanda chini ya utawala wa Kagame, ikifuatiwa na USA, UK na South Africa. Lakini kupitia utawala dhaifu wa Tshekedi kule DRC, taifa hilo la DRC likaamua kutaka kugawa migodi yake kwa kandarasi rasmi za uwekezaji za makampuni yale yale ya Belgium, USA, UK na South Africa jambo ambalo litaua mpango wa Rwanda kuendesha vita kule DRC (maana sponsor wake wamekimbia) kwa ujanja na uharaka Kagame akaamua kutengeneza deal jipya na China na baadaye Russia na hapo akaongeza nguvu kwa M23 kuongeza udhibiti wa maeneo zaidi kule DRC.
Chokochoko zikazidi na sasa zimeshika kasi, na rasmi sasa Kagame katangaza vita ya kidiplomasia dhidi ya jumuiya ya Ulaya kwa kuvunja uhusiano na taifa la Belgium ambalo lina nguvu za kiushawishi katika ulaya.
Kwa sasa Rwanda na Kagame wajiandae kwa mambo haya;
1. Kutengwa kimataifa hususani na ulaya na Marekani.
2. Kuwekewa vikwazo vya kiuchumi (Hata hii Tanzanite anayoivuna hapa Tanzania kwa wingi anaweza kukosa pa kuiuza)
3. Kukosa washirika muhimu wa kibiashara (usishangae hata Bandari za Dar, Mombasa, Beira, Djibout zikazuiwa kushusha au kupandisha Cargo za kibiashara na kijeshi za Rwanda)
4. Kutengenezewa mashtaka ya mauaji ya kivita ili kushtakiwa kwenye mahakama ya kimataifa.
5. Rwanda kuyumba kiuchumi, kitalii, Kidiplomasia.
6. Harakati za kumchafua kimataifa na kumpindua kuanzishwa.
Wewe ndugu yetu huwa unaitetea Rwanda kimkakati sana.Sidhani kama kutimuliana maofisa wa kibalozi kati ya Rwanda na Ubelgiji ni kwamba Rwanda wametangaza vita.
Ubelgiji hawakupaswa kuamua wawe upande upi wa mgogoro huu bali ni kuwa "neutral" na kujaribu kutatua tatizo, wao wameamua kuwa upande wa Congo DRC ambayo raisi wake ameishi Brussels akipikwa kuwa raisi kibaraka.
Pili, Rwanda si wajinga hivyo kuchukua uamuzi huo kwani wametoa sababu kadhaa ikiwemo ya Ubelgiji kuendeleza tabia za kikooni katika kushughulikia matatizo ya Rwanda na Congo DRC.
Hata EU wameweka vikwazo vya kiuchumi kwa Rwanda lakini vikwazo hivyo haviguzi sekta muhimu za viwanda uwekezaji na utalii ambapo bado nchi hiyo yaendelea kuwa na Uchumi Imara unokuwa huku kistratejia ikiimarisha mahusiano ya kiuchumi na kijeshi kwa nchi mbadala za mabeberu kama vile Qatar, Singapore na Uturuki hivyo kufanya utegemezi kuwa una mbadala kwa nchi za kibeberu.
Na mwezi jana CEOs kutoka nchi kadhaa za Afrika walikuwa mjini Kigali kuhudhuria mkutano mkubwa wa uwekezaji Katika teknolojia ya kifedha na pia kulikuwa na tour of Rwanda (ya kweli) ambayo ilivutia wageni lukuki.
Hivyo kufungiana ubalozi na kuwekewa vikwazo vyaweza kuwa ndo nyenzo muhimu lakini zisizo na matokeo mabaya sana kwa Rwanda.
Hata hivyo mimi siungi mkono vita wala kinoendelea huko Congo DRC na M23 kwai mamia ya watu wauliwa bila hatia lakini ni lzama kupatikane suluhisho kupitia majadiliano ambayo hayachagui upande wowote na ni lazima madai ya M23 yasikilizwe na uongozi wa Congo DRC.
✌️📌💯Ingekuwa jambo la busara na hekima sn kama wangemuua Kagame
Atakufa tu kama mimi na wewe tunavyosubiri. Usimfanye mungu mtu.Kagame hawezi kupinduliwa au kuuawa.
PK anasema ukimpiga kofi, ujiandae kurudishiwa makofi popote atakapoweza kukupiga. Ngoja tuone atakapomtandika Mbelgiji.Wewe ndugu yetu huwa unaitetea Rwanda kimkakati sana.
Nilidhani ni uchangiaji wa kuelewa dunia jinsi inavyokwenda, ila nilishangaa kwenye uzi wa muda mrefu mwanajeshi mstaafu wa Jwtz alivyokuwa anatoa simulizi ya vita kati ya Tanzania na Uganda bado ulikuwa unaizungumzia Rwanda kimkakati sana.
PK ameshasema huko wajifunge mkanda. Lakini kama kawaida yako uchangiaji wako kuhusu Rwanda unakuwa wa kimkakati sana.
Anatapa tapa tu wala hana athari yoyote. Soko lake kubwa la madini anayoyaiba Congo kuingia bara Ulaya yanapitia Ubelgiji.PK anasema ukimpiga kofi, ujiandae kurudishiwa makofi popote atakapoweza kukupiga. Ngoja tuone atakapomtandika Mbelgiji.
Wewe ndugu yetu huwa unaitetea Rwanda kimkakati sana.
Nilidhani ni uchangiaji wa kuelewa dunia jinsi inavyokwenda, ila nilishangaa kwenye uzi wa muda mrefu mwanajeshi mstaafu wa Jwtz alivyokuwa anatoa simulizi ya vita kati ya Tanzania na Uganda bado ulikuwa unaizungumzia Rwanda kimkakati sana.
PK ameshasema huko wajifunge mkanda. Lakini kama kawaida yako uchangiaji wako kuhusu Rwanda unakuwa wa kimkakati sana.
mazungumzo si ndiyo?Suluhisho la mgogoro wa Congo DRC, M23 na Rwanda litapatikana kutokana na nchi hizo kuzungumza.
Tumeishaona leo maraisi Tshisekedi na Kagame wamekutana uso kwa uso mjini Doha nchini Qatar kwa mazungumzo ambayo yameandaliwa na nchi hiyo ya Qatar ambayo ni nchi rafiki wa kistratejia wa Rwanda.
Hiyo ni moja ya hatua kubwa na nzuri iloanza kuchukuliwa ya nchi za Afrika kutatua migogoro inowahusu kati ya wao kwa wao.
Likija suala la hawa wakoloni wa zamani Ubelgiji na walokifanya Katika mkutano wa Berlin 1884-1885 ni kuligawa vibaya bara letu na kwa malengo ovu dhidi ya Afrika.
Tusishangae leo yanotokea Goma, Bukavu, Kivu ya kaskazini na Kivu ya Kusini maeneo ambayo kijiografia yameanza kuleta masuali mengi.
Hivyo mgogoro huu si wa kuutatua kwa kuchagua pande na wala kuingiliwa na wakoloni wa zamani bali ni mazungumzo ya kweli baina ya Congo DRC na Rwanda.
Hivyo hii jiografia ya siasa ya sasa yahitaji uelewa wa kurudi kwenye mkutano ule ili kuelewa hali ya sasa na yanotokea wakati huu na nini suluhisho lake.
Kwa sababu EU wameweka vikwazo katikati ya mazungumzo hivyo kuanza kuharibu.mazungumzo si ndiyo?
btw, kwanini kagme amekataa Kwenda angola?