Kagera: Chuo cha Kilimo cha Igabiro chasema Vyeti vya Wahitimu vimetoka na vinapatikana chuo

Kagera: Chuo cha Kilimo cha Igabiro chasema Vyeti vya Wahitimu vimetoka na vinapatikana chuo

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Baada ya Mwananchi ambaye ni Member wa JamiiForums.com aliyejitambulisha kuwa Mhitimu wa Igabiro Training Institute of Agriculture Wilayani Muleba kueleza kuwa Wahitimu wa awamu mbili chuoni takribani miaka miwili hawajapata vyeti licha ya kukamilisha taratibu zote, hatimaye vyeti vimetolewa.

Kusoma hoja ya awali, bofya hapa ~ Chuo cha Kilimo cha Igabiro (Kagera) chakiri Wahitimu hawajapata vyeti kwa miaka miwili, chasema ni suala linalohusu mamlaka za Serikali

Akizungumza na JamiiForums, Mkuu wa Chuo, Sadoki Stephano amesema “Vyeti vimetoka na vipo chuoni kwa sasa, Baraza limekamilisha mchakato wote na wanaohitaji wanakaribishwa kuja kuvichukua.

“Wanafunzi wote waliohitimu hapa wa Mifugo waje wachukue vyeti vyao kwa awamu zote mbili ambao walikuwa hawajapata. Upande wa Kilimo wao hawana changamoto.”

Vyeti vimetolewa kwa wote waliokidhi vigezo wale ambao walikuwa hawajakamilisha masomo wao bado.”

Pia soma ~ Chuo cha Kilimo cha Igabiro (Kagera) chakiri Wahitimu hawajapata vyeti kwa miaka miwili, chasema ni suala linalohusu mamlaka za Serikali
 
Mpaka mtu anaweka kwenye mitandao kulalamika ndio wanawajibika kweli hapo Kuna tatizo kubwa
 
Back
Top Bottom