Kagera: Gari la Hakimu lachomwa moto na wasiojulikana, Hakimu mwenyewe afunguka

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Mkuu wa Wilaya ya Muleba, Toba Nguvila amelitaka Jeshi la Polisi wilayani humo kufanya uchunguzi na kuwakamata watu ambao hadi sasa hawajafahamika, waliochoma moto gari aina ya Harrier lenye namba za usajili TI70 DEA.

Gari hilo, mali ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Mwanzo Nyamiranda, Kata ya Kyebitembe wilayani humo, lililochomwa moto usiku wa kuamkia Mei 11, 2022.

Akizungumza na baadhi ya wananchi wa kata hiyo katika eneo la tukio, mkuu wa wilaya huyo alisema matukio ya uhalifu katika kata hiyo yamekithiri na anasubiri kupata taarifa za kukamatwa kwa watu hao ili hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yao.

"Wapo baadhi ya wananchi wanatoa taarifa juu ya watu waliohusika, mwenyekiti nimeshakueleza na baadhi ya namba za simu nimekupatia, ninachokitaka ni kusikia hawa watu wote waliohusika wamekamatwa na kufikishwa katika vyombo vya sheria, wakipatikana tu nipewe taarifa," aliagiza.

Alisema Serikali haiwezi kuacha uhalifu uendelee katika kata hiyo maana hakuna mtu ambaye yuko juu ya sheria.

"Leo limechomwa gari la hakimu, kesho litachomwa la kwako mwenyekiti wa kijiji na keshokutwa litachomwa la mtendaji, ifikie hatua watu: watii sheria, vinginevyo vitendo hivi havitavumiliwa," alionya.

Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Mwanzo Nyamiranda, Emmanuel Jonathan, aliyechomewa gari lake, alidai hana ugomvi na mtu yeyote na hakuna mtu aliyejitokeza wazi kuo-:nyesha chuki dhidi yake.

Alisema kuwa pengine tukio hilo limefanywa na watu ambao hawakuridhika na uamuzi uli otolewa katika mahakama hiyo na hivyo kuamua kuchoma gari lake moto.

"Usiku nikiwa nimelala, walikuja baadhi ya wafanyakazi wetu wakiita kwamba 'amkeni gari limechomwa moto, tokeni kwenye nyumba, nayo inaweza kuungua'. Tukaamka na kutoka nje, tukaanza kutoa baadhi ya vitu nje lakini hatukuliokoa gari maana lilikwishateketea," alisimulia Hakimu Jonathan.

Alisema kuwa baada ya kufuatilia, waligundua kuwa watu hao walipitia katika shamba la migomba kwenda kuchoma gari na baada ya kuchoma gari hilo kwa kutumia mafuta ya Petroli walipitisha shamba hilo pia wakati wa kuondoka

Nipashe
 
Hii kesi ipelekwe mahakamani
 
Back
Top Bottom