Kagera: Kisa cha Mtoto mwenye Ualbino kudaiwa kuibiwa, RPC Makungu asema tayari wameanza uchunguzi

Kagera: Kisa cha Mtoto mwenye Ualbino kudaiwa kuibiwa, RPC Makungu asema tayari wameanza uchunguzi

Nyakijooga

JF-Expert Member
Joined
Dec 9, 2018
Posts
276
Reaction score
473
Kufuatia tukio la wa wasiojulikana kummyakua mtoto wa miaka miwili na nusu mwenye ualbino aitwaye Asiimwe Novath, na kutokomea naye, baada ya kumkaba koo mama yake anayefahamika kwa jina la Kebyera Richard, mkazi wa Kijiji cha Bulamula, Kitongoji cha Mbale, Kata na Tarafa ya Kamachumu wilayani Muleba mkoani Kagera.

Jirani wa familia hiyo, Hamad Rashid amesema kuwa tukio hilo lilitokea Mei 30,2024 muda wa saa 2:15 usiku.

Ameeleza kuwa vijana wawili ambao hadi sasa hawajafahamika, walifika nyumbani hapo kwa Kebyera, wakapiga hodi na kuomba chumvi. Walidai kuwa mwenzao amegongwa na nyoka; hivyo walitaka kumpa matibabu ya dharura kwa kutumia chumvi.

Rashid anasema, mama wa mtoto huyo ambaye wakati huo alikuwa nyumbani na mtoto wake, alifungua mlango na kuwapelekea chumvi huku akiwa amewasha tochi ya simu.

Wakati anawapa chumvi, mmoja wao alimkamata mama huyo na kumkaba koo; huku mwenzake akiingia ndani kwa haraka na kumchukua mtoto aliyekuwa akicheza sebuleni; na akatokomea naye kusikojulikana.

Wakati huo kijana aliyekuwa amemkaba mama wa mtoto huyo, baada ya kuona mwenzake ameshamkwapua mtoto na kutoka naye nje, alimwachia mama huyo na kukimbia, huku mama mtoto akibaki kupiga yowe kuomba msaada kwa majirani.

Baada ya wananchi kusikia yowe na kukusanyika nyumbani kwa Kebyera, walipiga simu polisi; na polisi walifika hima, kufanya mahojiano na kuanza upelelezi.

Bibi wa mtoto huyo, Odina Richard, ambaye anaishi Kanoni Kata ya Kamachumu, amesema kuwa alipigiwa simu na Kebyera binti yake – saa 2:30 usiku, na kuelezwa tukio lilivyokuwa.

Bibi huyo anasimulia kuwa bintiye alimweleza kuwa ilikuwa muda huo wa saa 2:15 wakati mume wake, Novati, hajatoka kazini, watu hao wasiojulikana waliposikika nje ya nyumba yao.

Anasimulia kuwa binti yake alimweleza kwamba kabla wanyang`anyi hawajapiga hodi, walianza kuita: “Mama Asiimwe! Mama Asiimwe” – kama majirani wanaofahamiana.

Mmoja wa watu hao wasiojulikana alikuwa akimwambia Mama Asiimwe kuwa amengongwa na nyoka mguuni na kwamba anaomba chumvi ili imsaidie kuondoa sumu.

Huku akibubujikwa machozi, Bibi Asiimwe haachi kupaza sauti na kauli za kujuta, akisema “inauma sana, inauma sana,” na kwamba hajui kama atamwona tena mjukuu wake. Anaomba Serikali imsaidie kumpata mjukuu wake akiwa hai.

Kwa upande wa Jeshi la Polisi kuipitia Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Gabriel Makungu amethibitisha kuwepo tukio hilo na kusema timu yake ya polisi imeanza uchunguzi juu ya tukio hilo.

Credit : Watetezi tv

=======

Mrejesho. 17/06/ 2024

Mtoto amekutwa amefariki huku mwili wake ukiwa umefungwa kwenye mfuko, pia baadhi ya viungo vyake vimepungua.

Pia soma:
 
Kama taifa tuliamua siasa ndio iwe kazi yenye malipo makubwa kuliko hata uprofesa wa chuo kikuu!

Matokeo yake ndio haya!!
 
Back
Top Bottom