Pre GE2025 Kagera: Matukio yanayojiri kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Pre GE2025 Kagera: Matukio yanayojiri kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760

WanaJF,

Mada hii itakuwa na 'Updates' za Matukio kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Urais, Ubunge na Udiwani 2025 kama yanavyotujia kutoka kwenu kutoka mkoa wa Kagera. Ukiwa na taarifa yoyote ambayo ni ya eneo hili tafadhali usisite kuweka.

1729461200220.png

Mgawanyiko wa Idadi ya Watu kwa Majimbo ya Uchaguzi Mkoa wa Kagera; Ramani ya Sensa ya Watu na Makazi ya 2022

Mkoa wa Kagera upo Kanda ya Ziwa katika Tanzania na ni maarufu kwa shughuli za kilimo na ufugaji, pamoja na Uvuvi. Mkoa huu una historia ya utajiri wa Ndizi na Kahawa. Madini yanayopatikana Mkoa wa Kagera ni Pamoja na chuma: dhahabu, bati ghafi, wolframite (WO3), Nickel, Manganese n.k

Idadi ya Watu

Matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 yanaonesha kuwa idadi ya watu katika Mkoa wa Kagera ni 2,989,299; wanaume 1,459,280 na wanawake 1,530,019.

Mkoa huu una Halmashauri nane (8) na majimbo ya uchaguzi tisa (9) ambapo Jimbo la Biharamulo Magharibi linaongoza kwa kuwa na watu wengi (457,114) likifuatiwa na Jimbo la Muleba Kusini (watu 442,652). Jimbo lenye idadi ndogo ya watu ni Bukoba Mjini ambalo lina watu 144,938, huku ukiwa na wilaya 8.

Idadi ya Majimbo ya Uchaguzi

Mkoa wa Kagera una jumla ya majimbo 9 ya uchaguzi:
  • Jimbo la Karagwe
  • Jimbo la Bukoba Vijijini
  • Jimbo la Bukoba Mjini
  • Jimbo la Muleba Kaskazini
  • Jimbo la Muleba Kusini
  • Jimbo la Biharamulo
  • Jimbo la Ngara
  • Jimbo la Kyerwa
  • Jimbo la Nkenge
HALI YA UCHAGUZI MKUU 2020

Mkoa wa Kagerra ulishiriki kikamilifu katika uchaguzi wa Rais, Wabunge, na Madiwani ambapo Chama Cha Mapinduzi (CCM) kiliibuka na ushindi mkubwa katika maeneo mengi ya mkoa huo.

Mgombea wa urais kwa tiketi ya CCM, Hayati John Pombe Magufuli, alipata kura nyingi zaidi kulinganisha na wapinzani wake.

Katika uchaguzi wa Ubunge, wagombea wengi wa CCM walishinda kwa kura nyingi dhidi ya wapinzani wao huku wakiwa na ushindi wa 100% kwa kuchukua majimbo yote Tisa

Uchaguzi wa Madiwani, (CCM) walipata ushindi mkubwa kwenye nafasi za madiwani ikifanikiwa kushinda kata nyingi. Hii ilitokana na upinzani kukumbwa na changamoto nyingi, zikiwemo wagombea wao kuenguliwa kutokana na matatizo ya kisheria au kutokidhi vigezo

Kulikuwa na malalamiko kutoka kwa vyama vya upinzani kama vile CHADEMA na ACT-Wazalendo kuhusu kutokuwepo kwa uwazi na haki katika mchakato wa uchaguzi.

Updates

February
March

ZINGATIA: Mikoa yote ina mada yake ya 'Update' ili kuweka wepesi katika ufuatiliaji.
 
Back
Top Bottom